Kuna waliomfata Lowassa Z’bar? Nape na TAKUKURU ilikuwaje?
NIPASHE
Wanachama wa CCM Zanzibar wamesema hawapo tayari kumuunga mkono Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kwa kitendo cha kukihama chama hicho na kujiunga na CHADEMA.
Katibu wa Mkoa wa Mjini CCM, Muhammed Nyawenga amesema Lowassa
asidhani kuwa wanachama wengi wa CCM walimuunga mkono wakati
alipotangaza nia ya kugombea Urais wa Muungano kupitia chama hicho,
akadhani kuwa na sasa watakuwa pamoja naye.
“Tunamwambia Lowassa kama mvuvi wa pweza basi tutakutana mwambani”– Muhammed Nyawenga.
Nyawenga amesema uamuzi wa Lowassa
kutoka CCM sio jambo la kukishtua chama, wanachama wala viongozi wa
chama hicho na kamwe CCM haiwezi kudhoofika wala kupasuka kwani sio mara
ya kwanza kwa CCM kuondokewa na kiongozi muandamizi na kujiunga na
upinzani.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa mjini Magharibi ambae alikuwa kinara katika kumuunga mkono Lowassa wakati akiomba ridhaa ya Chama hicho kugombea Urais kupitia CCM, Borafya Silima Juma amesema kiongozi huyo anapenda madaraka na ukubwa na ndio maana baada ya jina lake kutopita ameamua kujiunga na CHADEMA.
NIPASHE
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Lindi imemhoji Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye kwa madai ya kukutwa na fedha zinazodaiwa za kuwapa Wajumbe ili wamchague katika kura za maoni.
Nape alikamatwa wakati akitoka ndani ya Benki na alipofika nje alikutana na askari wa kikosi hicho na kumuweka chini ya ulinzi.
Maofisa hao walimchukua kwa mahojiano
ofisi ya TAKUKURU yaliyochukua saa tano, kuanzia saa 4:30 asubuhi hadi
saa 9:30 alasiri na kuachiwa.
Waandishi wa habari waliokuwepo eneo hilo, walishuhudia askari hao wakimkamata na Nape kujaribu kupinga.
“Mheshimiwa sisi ni askari wa TAKUKURU , usijivunjie heshima tunakuomba uongozane na sisi kuelekea ofisini kwetu,” alisema mmoja wa askari hao.
Waandishi wa habari walipomhoji Nape
kuhusu tuhuma hizo, alikiri kwenda ofisi hizo, lakini alikataa kueleza
alichoitiwa na kudai alikwenda kwa ajili ya matembezi yake binafsi.
“Mimi sikuhojiwa na Takukuru ila nilikwenda kwa matembezi yangu binafsi,” alisema Nape.
Kamanda wa Taasisi hiyo, Stephen Chami
alipotakiwa kuthibitisha tuhuma hizo, aliwataka waandishi wafanye
subira kwani wapo katika mahojiano nae, baada saa nne kupita, alipigiwa
tena simu na kukiri kumhoji Nape, katika mahojiano hayo Nape alisema fedha hizo alizichukua kwa ajili ya kuwalipa Mawakala.
Nape
ametangaza nia ya kugombea jimbo la Mtama mkoani Lindi ambalo kwa sasa
linashikiliwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.
HABARI LEO
Wanachama wa CCM na Chadema wa familia mbili tofauti wamepigana na kuumizana vibaya wakizozana kuhama katika vyama hivyo.
Mkasa huo ulitokea juzi katika Kijiji
cha Nondo Wilaya ya Kalambo Mkoa wa Rukwa baada ya Wagombea Udiwani
wa CCM kumaliza kikao chao, wakiwaomba wanachama wenzao wawachague
katika kura ya maoni.
Ugomvi huo ulihusisha familia ya Katibu Mwenezi wa CCM wa kata hiyo, Meidi Sinkamba na mwanawe Hamoud Milambo na familia ya mwanachama wa CHADEMA, Waton Silawe na mwanawe Megji Silawe.
Ilidaiwa kuwa Megji alianza kumshambulia
kwa maneno Katibu huyo Mwenezi wa CCM akihoji kwa nini amewaleta
madiwani hao wa CCM kujinadi kijijini kwao wakati wanachama wa CHADEMA
wakifurahia aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa kujiunga rasmi na chama hicho.
Malumbano hayo ya maneno yalimkasirisha Hamoud ambaye aliingilia kati ili kumsaidia mama yake mzazi huku Mzee Kasomo naye akimtetea mwanawe Megji.
MTANZANIA
Wanafunzi wa Shule za Msingi Kisiwa kilichopo Ukerewe Mwanza wanasoma kwa zamu kutokana na ukosefu wa madarasa.
“Hali
ya Wanafunzi kupata elimu ni jambo la msingi lakini miundombinu
hairidhishi, shule yetu ina majengo mawili yenye vyumba vine vya
madarasa, wanafunzi wanasoma kwa zamu”—Mwenyekiti wa Kitongoji, Muzumari Kasanzila.
Mwenyekiti huyo amesema Diwani wa Kata yao amehamia Morogoro na Mbunge Salvatory Machemuli hajafika muda mrefu kisiwani hapo hivyo hajui matatizo ya Wananchi wake.
HABARI LEO
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara, Rajab Luhavi
amesema hakuna utaratibu wa kikanuni wa kumzungumzia mwanachama
anayekihama chama hicho na kuwa wanajiandaa na siasa za kiushindani ili
kulinda hadhi na heshima ya CCM.
Naibu Katibu Mkuu huyo amemtakia kila la heri Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa aliyehamia CHADEMA.
Luhavi amesema
suala la kuzungumzia mwanachama anayehama limekuwa la mazoea tu, na
siyo la kikanuni rasmi na kwamba mara nyingi wanapoondoka hawasemi, bali
huzungumza wanaporejea katika chama hicho.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment