Ukaaji huu kwenye ndege ilikuwa tatizo kwa mtu wa pembeni, mambo yamebadilika.. Kilichofuatia je??
Kampuni ya ndege ya Etihad iliyopo Abu Dhabi imeingia kwenye headlines baada ya abiria James Bassos kuishitaki kampuni hiyo kwa matatizo ya mgongo yaliotokana na kupangiwa siti karibu na mtu mnene.
Documents zilizopelekwa Mahakamani na James Bassos zina maelezo kwamba wakati akiwa safarini kutoka Dubai kwenda Sydney mwaka 2011 alilazimika kujigeuza geuza na kujibana ili kuzuia kugusana na mwenzake ambae mwili na uzito wake ni mkubwa kupita kiasi.
Licha ya
kuomba kuhamishwa siti zaidi ya mara moja na wahudumu wa ndege hiyo,
ombi lake ni kama hakuna aliyejali kumsaidia zaidi ya kumpa ushauri
kwamba kama akijisikia maumivu ainuke kujinyoosha nyoosha kidogo
!!.. badaae akashuka akiwa na maumivu makali sana ya mgongo.
Kesi hiyo dhidi ya ETIHAD bado
inaendelea lakini kama Kampuni hiyo ya ndege ikikutwa na hatia basi
kampuni hii itakuwa imevunja sheria kuu ya kampuni yao inayosema “usalama na faraja ya abiria wa Etihad Airways ni suala la umuhimu kwetu…”
Kampuni ya ETIHAD
hii ni mara ya pili inaingia kwenye headlines zisizopendeza, ni April
2015 walitajwa kumfukuza kazi mfanyakazi mwanamke mmoja kwa sababu
alikuwa mjamzito !!
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment