Tangakumekuchablog
Moshi,
WAANDISHI wa habari nchini wametakiwa kuandika habari kwa usahihi wakati wa
uchaguzi mkuu mwaka huu na kuepuka kushabikia vyama na wagombea jambo ambalo
linaweza kuwa chanzo cha kuharibika kwa amani.
Nasaha hizo zilitolewa jana na
Mwandishi mwandamizi, Atilio Tigalile wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari
kanda ya Kaskazini yaliyofanyika Mkoani Kilimanjaro na kuitishwa kwa pamoja na
Baraza la Habri la Taifa (MCT) na BBC
Media Action.
Alisema mara nyingi waandishi wa
habari nyakati za chaguzi wamekuwa wakiingia katika misuguano na vyama baada ya
kuandika habari za upande mmoja na hivyo kuwataka kubadilika na kurejea katika
maadili yao ya kazi.
Alisema mwandishi wa habari anapaswa
kuzingatia taaluma yake ya upashaji wa habari na kuepuka vishawishi vya
kuandika habari upande mmoja na kuacha kurubuniwa kwa vitu vidogo.
“Nawaomba ndugu zangu waandishi wa
habari muliopata nafasi ya kuwepo hapa na wale ambao hawapo----jiepusheni
kuandika habari za upande mmoja na kuepuka kudanganyika na vitu vidogo vidogo” alisema Tigalile
na kuongeza
“Zingatieni maadili yenu ya habari
kwa kuandika kwa weledi kwani kutawafanya kuwa salama na uwepo wenu popote
muendapo kuchukua habari za wagombe wakati wa kampeni” alisema
Alisema mwandishi wa habari anaweza
kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani endapo atakiuka maadili ya kazi yake na hivyo
kuwataka kuepuka kufanya hivyo na kurejea katika mstari wa ukweli na uhuru
usiopitiliza mipaka.
Kwa upande wake, Mwandishi wa siku
nyingi, Kyondo Mshana, aliwataka waandishi hao kuyatumia mafunzo hayo na kuwa
mfano wa kuingwa kwa waandishi wengine wa vyombo vya habari.
Alisema kuandika habari kwa usahihi
kutamfanya mwandishi kuwa salama wakati wowote na pahala popote na hivyo
kukisaidia chombo chake jambo ambalo linaweza kukiletea sifa chombo chake
anachofanyia kazi.
“Kuandika habari kwa usahihi
kutawafanya kuwa huru na salama jambo ambalo chombo chako unachofanyia kazi
kuaminika na kupendwa jambo litakalowafanya walaji kulipenda” alisema Mshana
Alisema kuelekea uchaguzi mkuu mwaka
huu mwandishi anatakiwa kuepuka vishawishi na kuzingatia maadili ya taaluma ya
habari ili kuepuka mizozo wakati anapoenda kufuata habari kwa vyama vyote
wakati wa kampeni hadi uchaguzi.
|
People (2)
|
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari kutoka kanda ya Kaskazini wakiwa katika mafunzo mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro jana juu ya kuandika habari za uchaguzi kwa Ukweli na Uwazi bila kuegemea upande wowote wa vyama wakati wa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Octobar mwaka huu. Mafunzo hayo yaliratibiwa kwa pamoja na Baraza la Habri la Taifa na BBC Media Action
No comments:
Post a Comment