Kama kuna ndoa ziliwahi kukushtua, nakuongezea na hii nyingine ya mtu na nyoka..

Ya leo itakushangaza pia.. eti ndoa ya binadamu na nyoka?
Iko kwenye HEADLINES toka India, inamhusu Sandeep Patel ambaye alipanga mikakati ya kumuoa nyoka aina ya cobra .. anasema huyo ndio mwanamke mrembo ambaye alikuwa na ahadi nae kwamba atamuoa siku ya Pasaka.
Watu walitaka hii isiwapite yani,
unaambiwa zaidi ya watu 12,000 walisogea kwenye hekalu ambako ndoa
ilikuwa inafanyika katika kijiji cha Badwapur, India.
Muda ulipofika taratibu zote zikaanza
kama kawaida.. mhubiri wa kihindi aliyekuwa anafungisha ndoa hiyo
aliwaambia watu kuwa jamaa huyo alikuwa anapenda nyoka tangu akiwa
mtoto.. alikuwa anatembea, anakula na kuchezesha ulimi wake kama
anavyofanya nyoka.
Polisi waliingia kwenye ukumbi huo
na kuzuia harusi hiyo isiendelee, wakawakamata bwana harusi pamoja na
baba yake.. alafu wakaanza kazi nyingine ya kuwatawanya watu wote
waliokusanyika kushuhudia tukio hilo la kihistoria.
Hii inafanana na ile nyingine ambayo imetokea Mexico, jamaa alikaa kwenye HEADLINES kwa kuoa mamba.
www.tangakumekucha inakuhabarisha kila linalotekea pembe zote za dunia peruz kila wakati ni hapa hapa
No comments:
Post a Comment