Tangakumekuchablog
Tanga, JAJI Mkuu
mstaafu, Augostino Ramadhani, amewataka viongozi wa dini kuyatumia majukwaa yao
kwa kuhubiri amani na kuvumiliana katika mambo ya dini hasa kipindi hiki cha
kuelekea uchaguzi mkuu mwaka 2015.
Akizungumza katika warsha ya siku
mbili ya mahusiano ya dini na amani ya nchi iliyofanyika mjini hapa leo, Augostino
aliwataka viongozi hao kuwahubiria wafuasi wao kuvumiliana katika mambo ya
dini kwani Watanzania utamaduni wao ni wa kuvumiliana.
Alisema kiongozi wa dini anaweza
kuwa chanzo cha kuvurugika kwa amani ikiwa mahubiri yake atachanganya dini na
siasa na hivyo kuwataka kuyatumilia majukwaa yao kwa kuwahubiria amani.
Alisema kuelekea uchaguzi mkuu ni
wajibu wa viongozi wa dini kuwataka wafuasi wao kushiriki katika uchaguzi kikamilifu kwa kuchagua viongozi waoona
wanafaa bila ubaguzi wa rangi dini wala
kabila.
“Nimefarijika kuwa mshiriki wa
warsha hii kuzungumzia amani ya nchi kwani imekuja muda muafaka kuelekea
uchaguzi mkuu mwaka huu tukiwa pamoja na viongozi wa dini mbalimbali” alisema
Ramadhani na kuongeza
“Sote tunatambua kuwa viongozi wa
dini wako na mchango mkubwa katika kuliweka Taifa letu katika misngi amani na
kuvumiliana----huu ndio utamaduni wetu na ndio maana nchi yetu inasifika
ulimwengini kote” alisema
Awali akifungua warsha hiyo, Mkuu wa
Mkoa wa Tanga, Said Magalula, aliwataka viongozi hao wa dini kuwa mabalozi
wazuri wa amani mara watakapomaliza mafunzo yao.
Alisema kipindi hiki cha kuelekea
uchaguzi mkuu viongozi wa dini wako na wajibu na haki ya kuwaelimisha wafuasi
wao umuhimu wa kushiriki uchaguzi mkuu ujao.
Alisema kushiriki katika uchaguzi ni
jambo muhimu kwani mpiga kura ataweza kumpata kiongozi anaemtaka na kuondosha
manung’uniko kwa kuchaguliwa kiongozi ambaye hakumpenda.
“Ndugu zangu viongozi wa dini ni
furaha yangu kuwa warsha hii itawajengea uwezo----ndugu zetu wourd vision
wameona umuhimu wa kulifanya jambo hili kwa lengo tu la kudumisha amani ya
nchi” alisema Mgalula
Alisema Wourd Vision imetambua
umuhimu wa amani hasa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu na hivyo kuwataka
kuyatumilia na kuwa mabalozi wazuri maeneo wanayotoka.
Mwisho
No comments:
Post a Comment