Uchambuzi huu wa magazeti unaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya kituo cha Elimu Cha Candle Education Centre Tanga, kituo kinaongoza kufaulisha wanafunzi kidato cha pili hadi cha sita kwa wale ambao wanarisiti Kituo pia kinatoa kozi ya Kiingereza na Computer. Wapo Tanga mkabala na Bank ya CRDB simu 0715 772746
Muswada wa Mahakama ya Kadhi umeondolewa
bungeni na sasa hautajadiliwa katika Mkutano wa 19 wa Bunge
unaohitimishwa leo mjini hapa.
Huu ni muswada wa tatu kuondolewa
Bungeni baada ya ile miwili ya sekta ya habari ambayo ni muswada wa
Sheria ya kupata Taarifa wa mwaka 2015 na ule wa sheria ya huduma wa
Vyombo vya Habari iliyoondelewa mwishoni mwa wiki iliyopita.
Muswada huo ulipangwa kuwasilishwa Bungeni leo, lakini serikali imeamua kuuondoa kutokana na hofu ya kutokea mpasuko nchini.
Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashilila, akizungumza jana ofisini kwake alisema muswada wa Mahakama ya Kadhi hautakuwapo tena katika mkutano huo.
Dk. Kashilila alisema haijulikani ni
lini utawasilishwa bungeni kwa sababu Mkutano wa Bunge ujao unaotarajia
kufanyika Mei, utakuwa mahsusi kwa ajili ya bajeti.
“Waziri
Mkuu alivyosema wataangalia na kushauriana kimsingi, alitoa maneno ya
busara tu au ilikuwa kauli ya mtu mzima, lakini huu muswada
hautakuwapo,” alisema.
Dk. Kashilila alisema hali iliyojitokeza
Jumapili iliyopita wakati wa semina ya wabunge haikuwa nzuri kutokana
na mvutano mkali miongoni mwa wabunge.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju,
alipoulizwa kuhusu kama muswada huo utawasilishwa bungeni, alisema
hakuwa na majibu badala yake alitaka suala hilo iulizwe ofisi ya Spika.
“Suala hili usiniulize, nenda Ofisi ya Spika au muulize huyu (Magati) ambaye yupo sekretarieti,” alisema huku akiwa na haraka kuelekea ofisini kwake.
Naibu Spika, Job Ndugai,
akizungumza nje ya ukumbi wa Bunge muda mfupi baada ya kuahirisha
Bunge, alisema muswada wa Mahakama ya Kadhi hautawasilishwa bungeni leo.
“Huo muswada hauwezi kuletwa bungeni kutokana na hali ilivyo,” alisema Ndugai bila kufafanua zaidi.
Naye Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Asha-Rose Migiro,
alipoulizwa kama muswada huo utawasilishwa bungeni alimtaka mwandishi
asimuulize maswali yanayohusiana na muswada wa Mahakama ya Kadhi.
“Sitaki kabisa kuulizwa suala la Muswada wa Mahakama ya Kadhi, kwanza wewe unatoka gazeti gani, “alijibu Dk. Migiro kwa hasira huku akiingia kantini.
Katika hatua nyingine, juzi jioni
maaskofu zaidi ya 40 kutoka mikoa yote nchini, walikutana na wabunge
katika ukumbi wa Kanisa La Kiinjili la Kilutheli (KKKT) mjini Dodoma kujadiliana suala la muswada wa Mahakama ya Kadhi.
Baadhi ya wabunge waliohudhuria mkutano
huo walisema kuwa katika mkutano, maaskofu walitoa azimio kuwa muswada
huo usiwasilishwe bungeni kwa kuwa hatua hiyo inaweza kuhatarisha amani
iliyoko nchini.
NIPASHE
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera
linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kukutwa na viungo vya mtu
mwenye ulemavu wa ngozi (albino).
Watu hao wanatuhumiwa kufukua kaburi la
mtu huyo na kuchukua kila kiungo cha mwili wa mtu huyo aliyejulikana kwa
jina la Bartazar John, aliyefariki mwaka 1991.
Hatua hiyo imechukuliwa na jeshi hilo
zikiwa zimepita siku saba tangu watu wengine wawili kutiwa nguvuni kwa
tuhuma za kuhusika kuuza viungo vya marehemu Wilaya ya Muleba, mkoani
humo.
Kamanda wa Polisi mkoani humo, Henry Mwaibambe,
alisema watu hao walikamatwa Machi 27, mwaka huu, katika nyumba moja ya
kulala wageni, iliyoko eneo la Kyaka, Wilaya ya Missenyi baada ya
kukutwa wakiwa na baadhi ya viungo hivyo, ambavyo walikuwa wanakwenda
kuviuza.
Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Laston Faustine (41), ambaye ni mkazi wa Lukulaijo aliyekutwa na mfuko uliokuwa umehifadhi mifupa mitatu ya binadamu na mwingine ni January Korongo (43), mkazi wa Kadengesho, wiyani Karagwe.
Kamanda Mwaibambe alisema baada ya
kumbana, mtuhumiwa wa kwanza, Laston aliliambia Jeshi la Polisi kuwa
aliyempa viungo hivyo ni mwenzake, January, kwa ajili ya kuviuza kwa Sh.
milioni 20.
Baada ya kuhojiwa, January alikiri
kufukua kaburi la mjomba wake, aitwaye Baltazari aliyekuwa na ulemavu wa
ngozi albino pia mlemavu wa viungo, ambaye alifariki dunia mwaka 1991
na walifukua kaburi lake mwaka 2009.
Mwaibambe alisema baada ya kumhoji zaidi
mtuhumiwa huyo, alikubali kuongozana na polisi hadi nyumbani kwake,
ambako alionyesha fuvu la kichwa, mifupa mitatu ya miguu pamoja na
mifupa ya sehemu mbalimbali, ambayo ilikuwa imefungwa kwenye mfuko nje
ya nyumba yake.
Polisi waliomba kibali cha Mahakama
Wilaya ya Karagwe kuruhusiwa kufukua kaburi hilo ili kuhakikisha kama
kweli kuna mabaki ya mwili huo, lakini hakuna kilichopatikana.
NIPASHE
Jukwaa la Wakristo Tanzania, limesema
linashangazwa na tabia ya baadhi ya viongozi wa serikali wenye tabia ya
kuitisha mikutano wanayoiita ni ya viongozi wa dini huku ikiwa siyo
rasmi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana
kwa vyombo vya habari na Jukwaa hilo, imeeleza kuwa viongozi hao
wamekuwa chanzo cha mvutano uliopo baina ya dini mbili na kwamba
watakuwa chanzo cha kuvurugika kwa amani nchini.
Taarifa hiyo ambayo imesainiwa na Mkuu Habari na Mawasiliano wa Baraza la Kikiristo Tanzania (CCT), Mchungaji John Kamoyo,
ilisema jopo la Maaskofu kutoka TEC, CPT lilikutana Machi 30, mwaka
huu, mjini Dodoma, kuondoa dhana kuwa linaongozwa na hasira na mihemko
katika kufikia maamuzi linavyoyafanya kama wengine wanavyotafsiri bali
linasukumwa kwa upendo wa wananchi ili kujenga taifa lenye umoja, amani,
utulivu na maelewano.
Kamoyo alisema Machi 03, 2015 Waziri
Mkuu aliitisha mkutano kupitia Mchungaji mmoja ambapo hakuna kiongozi wa
taasisi au Kanisa aliyeshiriki, na kwamba Machi 28, mwaka huu, Rais
Jakaya Kikwete, alikutana na kikundi ambacho sio rasmi yaani Kamati ya
Amani ya Mkoa wa Dar es Salaam.
“Maaskofu tuliokutana Dodoma hatuongozwi
na hasaira wala mihemko katika kufanya uamuzi kama wengine
wananavyotafsiri, tunafikia uamuzi baada ya maombi kwa upendo wa
wananchi na kujenga taifa lenye umoja na amani,” alisema Mchungaji
Kamoyo.
Kamoyo alisema walikewenda Dodoma
kufuatilia kwa kina Muswada wa Sheria mbalimabali za mwaka 2014 pamoja
na mrekebisho mengine ya Sheria ya Tamko la Sheria za Kiislamu la mwaka
1964.
MWANANCHI
Siku tano baada ya Rais Jakaya Kikwete kusema kuwa tamko la Jukwaa la Wakristo (TCF)
kuwataka waumini wao kupigia kura ya ‘hapana’ Katiba Inayopendekezwa
lilikuwa la hasira, viongozi hao wamejitokeza tena na kusisitiza kwamba
msimamo wao huo utabaki kama ulivyo.
Katika tamko pamoja walilolitoa jana
baada ya kukutana juzi mjini Dodoma, viongozi hao wamemtahadharisha Rais
Kikwete kuwa kuendelea kupigia debe Katiba Inayopendekezwa na kuruhusu
Mahakama ya Kadhi, kunaweza kulitumbukiza Taifa katika machafuko na hali
ikiwa hivyo Serikali ndiyo itakayolaumiwa.
Tamko hilo limesainiwa na viongozi
walewale waliosaini lile la awali la Machi 12, mwaka huu ambao ni
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Askofu Dk Alex Malasusa, Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa na Mwenyekiti wa Kanisa la Pentekoste Tanzania (CPCT), Askofu Daniel Awet.
Tamko hilo la maneno 921, limeendelea
kuwataka waumini wao kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika Daftari
la Kudumu la Wapiga Kura, kuisoma Katiba Inayopendekezwa na kujitokeza
kuikataa kwa kupiga kura ya ‘hapana,’ msimamo ambao tayari umeibua
msuguano baina yao na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es
Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo aliyesema viongozi wa dini hawana mamlaka ya kuwaamulia waumini wao aina ya kura wanayostahili kupiga.
Pia, Jukwaa hilo limewataka viongozi wakuu wa Serikali –Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
na Rais Kikwete wasifurahi kwamba ujumbe wao umewafikia viongozi wa
dini waliozungumza nao hivi karibuni, kwa kuwa watu waliokutana nao si
wawakilishi rasmi na hawana uwezo wa kutoa uamuzi au kukubaliana juu ya
jambo la kitaifa.
“Maaskofu
tuliokutana hapa (mjini Dodoma) hatuna hasira na wala hatuongozwi na
hasira wala mihemko katika kufikia maamuzi tunayofanya kama ambavyo
wengine wanavyotutafsiri, tunafikia maamuzi yetu baada ya maombi na sala
na tunasukumwa na upendo kwa wananchi ili kujenga Taifa lenye umoja,
amani, utulivu na maelewano,” lilisema tamko hilo likihitimishwa kwa
maneno ya Biblia kutoka Mithali 29: 1, “Aonywaye mara nyingi akishupaza
shingo, atavunjika ghafla, wala hapati dawa.”
Jumamosi iliyopita, Rais Kikwete
akifungua mkutano wa Kamati ya Amani ya Mkoa wa Dar es Salaam
iliyoshirikisha wajumbe kutoka mikoa mbalimbali ikijumuisha viongozi wa
dini za Kiislamu na Kikristo, alisema msimamo wa TCF kuhusu kuipigia
kura ya ‘hapana’ Katiba Inayopendekezwa ni wa hasira na usiokuwa na tija
kwa maendeleo ya Taifa.
“Nimeyasoma
matamko hayo yote kwa umakini, imenishangaza, imenisikitisha na
kunihuzunisha. Siamini kwa nini wamefikia huko kwa kuunga au kutokuunga
mkono,” Rais Kikwete.
Rais Kikwete alisema: “Waacheni
waumini waamue Katiba wanayoitaka wao… hayo matamko niliyoyasoma
yamejaa hasira kwa Serikali kupeleka bungeni Muswada wa Mahakama ya
Kadhi.”
Maaskofu hao walikuwa Dodoma kufuatilia
kwa kina Muswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali ya mwaka 2014
unaopendekeza, pamoja na mambo mengine, marekebisho ya Sheria ya Tamko
la Sheria za Kiislamu la mwaka 1964 unaotambua Mahakama ya Kadhi.
“Muswada
huu unapendekeza kuanzishwa Mahakama ya Kadhi ambao utawasilishwa
bungeni leo kwa hati ya dharura na hivyo kuufanya umma wa Watanzania
kutokujua maudhui yaliyomo katika muswada huo wakati bado hoja zetu za
msingi tulizopeleka kwenye Kamati ya Katiba na Sheria ya Bunge na kwa
Waziri Mkuu hazijajibiwa,” Ilieleza taarifa hiyo.
MWANANCHI
Askari polisi wawili wameuawa na mmoja
kujeruhiwa baada ya kuvamiwa na watu wanaodhaniwa kuwa na viashiria vya
ama ugaidi au ujambazi katika kizuizi cha barabara ya Kilwa, Kipara
Mpakani, Wilaya ya Mkuranga, mkoani Pwani.
Tukio hilo ambalo tayari limelaaniwa na
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe na Tume ya Utawala
Bora na Haki za Binadamu, limekuja katika kipindi ambacho Mkuu wa Jeshi
la Polisi (IGP), Ernest Mangu amepangua makamanda na maofisa wa polisi 160 nchini kote.
Wakati Polisi Kanda Maalumu ya Dar es
Salaam ikisema inachunguza chanzo cha vifo vya askari hao ambao ni wa
kanda hiyo, Chikawe alisema tukio hilo linawezekana kuwa la kigaidi au
ujambazi lenye lengo la kuchukua silaha kwenda kufanyia matuko
mbalimbali.
Askari waliouawa ni D.2865 SGT Francis na E.177 CPL Michael wakati aliyejeruhiwa ni D 5573 D/SGT Ally.
Walioshuhudia tukio hilo walisema
lilitokea juzi saa mbili usiku na kudumu kwa dakika 10 na kufanya eneo
hilo kuwa kama uwanja wa vita kutokana na milio ya risasi.
Mkazi wa eneo hilo, Mohamed Ali alisema aliwaona watu watano wakitokea katika Pori la Kipara Mpakani, mmoja akiwa ameshika bunduki na mwingine panga.
“Niliwaona
wakiwafuata askari karibu na kizuizi, mmoja alimpiga polisi risasi
kifuani na mwingine akamkata polisi kwa panga shingoni,” alisema na
kuongeza kuwa aliwaona askari hao wakiwa wamelala chini baada ya kuuawa…
“Baada ya tukio hilo, watu wote waliokuwa karibu na eneo hili
walikimbia kujificha wakihofia usalama wao.”
Shuhuda mwingine, Shiraz Abdul alisema alimwona mmoja wa askari mwingine akikimbia pamoja na wananchi baada ya tafrani hiyo… “Niliwaona askari watatu wakiwa wamelala chini, mmoja akiwa analia kuomba msaada,” aliongeza.
Shuhuda, Rehema Yusuph ambaye anaishi
karibu na barabara kilipo kizuizi hicho alisema, walianza kusikia watu
wakipiga kelele na kuhisi kwamba ilikuwa ajali.
“Mara
nyingi huwa ajali zinatokea hapo barabarani, kwa hiyo sisi tulidhani
kwamba ilikuwa ajali. Lakini baada ya sekunde chache tulianza kusikia
milio ya risasi. Mara nikaona watu wanakimbilia kwenye veranda yangu,
baada ya kuuliza wakasema kuna watu wamevamia hicho kituo na wameua na
kujeruhi askari.”
MTANZANIA
Ni maumivu. Ndivyo unavyoweza kusema baada ya Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima kutoka Hospitali ya TMJ alikokuwa amelazwa kwa siku tano kwa kutumia baiskeli ya wagonjwa (wheelchair) kwenda Kituo cha Polisi Oysterbay kuhojiwa kwa mara ya pili.
Askofu Gwajima, alipandishwa kwenye
baiskeli hiyo, baada ya kupelekewa na mmoja wa wafuasi ambaye alikuwa
amevalia mavazi ya kichungaji.
Wakati akipelekwa katika gari Askofu
Gwajima, alionekana akigugumia kutokana na maumivu makali ambayo
haikujulikana mara moja chanzo chake.
Baada ya wafuasi wake kukamilisha
taratibu zote, ilipofika saa 6:15 mchana, gari la polisi aina ya Land
Cruiser lenye namba za usajili KX 06 EFY liliwasili hospitalini hapo.
Gari hilo, lilikuwa na askari wanne,
mmoja akiwa ni ofisa wa polisi aliyekuwa amevalia sare za askari wa
Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) na wengine wakiwa wamevalia kiraia.
Askari hao ambao walikuwa wamebeba bunduki walikwenda moja kwa moja wodini na baadae kutoka pamoja na kiongozi huyo wa kiroho.
Baada ya muda kidogo, askari hao
walishuka chini na ilipofika saa 06:34 chana, gari nyingine ndogo aina
ya Yutong MG 6 Turbo yenye namba STL 110 iliwasili eneo hilo ikiwa na
askari mmoja.
Ilipofika saa 6:45, Askofu Gwajima
alishushwa katika lifti ya hospitali hiyo, akiwa anasindikizwa na zaidi
ya watu wane, huku yeye akiwa amekaa kwenye baiskeli hiyo na kupandishwa
moja kwa moja kwenye gari la polisi.
Akiwa anainuliwa kwenye kiti na
kupandishwa katika gari, Askofu Gwajima alionekana akikunja uso na
kufungua mdomo kama mtu anayegugumia kutokana na maumivu makali.
Baada ya kutoka hospitalini, msafara huo ulielekea moja kwa moja Kituo cha Polisi cha Oysterbay.
Alifikishwa kituoni hapo saa 6:55 na kupelekwa chumba kilichokuwa kimeandikwa ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Kinondoni.
Alipofika mlangoni alikutana na ofisa
mmoja, ambaye jina lake halikutambuliwa mara moja, alimuaru asubiri ili
wakili wake afanye taratibu za dhamana.
“Subiri
hapa mfanye taratibu za dhamana mkishamaliza hakikisha Alhamisi (kesho)
unaripoti Central Polisi (kituo kikuu cha polisi Dar es Salaam),”alisikika ofisa huyo akisema.
Wakati taratibu za dhamana zikiendelea,
wafuasi wa Askofu Gwajima waliendelea kukusanyika eneo hilo kwa madai
kuwa wanamsubiri kiongozi wao.
Wakiwa wamekusanyika makundi makundi,
huku wengine wakiwa wameshikilia makaratasi yenye maandishi na picha
ndogo kwa ajili ya kusaidia udhamini kama ukihitajika.
MTANZANIA
Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) umelaani na kusikitishwa na kauli za viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF) kuitupia lawama CCM kwa kudai imehusika katika kushambuliwa wafuasi wao.
Wakati CCM wakitoa kauli hiyo, CUF kimemtupia lawama Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK), Balozi Seif Ali Idd kuwa ndiye amekuwa akitoa kauli za kuchochea vurugu visiwani humo.
Taarifa ya UVCCM Zanzibar kulaani
matamshi hayo ilitolewa jana kwa vyombo vya habari na Naibu Katibu Mkuu
wake, Shaka Hamdu Shaka.
Wafuasi wa CUF walivamiwa na kupigwa na
watu wanaodaiwa kuwa wanachama wa CCM, ambapo katika vurugu hizo watu 25
waliokuwa wakitokea katika mkutano uliokuwa unafanyika Makunduchi
Wilaya ya Kusini Unguja walijeruhiwa.
Shaka alisema katika taarifa yake kwamba
baadhi ya viongozi wa CUF wakiwamo wawakilishi wa chama hicho, kwa
nyakati tofauti wamesikika na kunukuliwa na vyombo vya habari wakidai
shambulio hilo la kudhuru limepangwa na kufanywa na vijana wa CCM jambo
alilosema si kweli na halina ushahidi.
“Shutuma za CUF kwa namna moja au
nyingine zimejiegemeza katika kuficha ukweli wa chanzo halisi kwani
itakumbukwa hivi karibuni Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif
Hamad katika moja ya mikutano yake ya hadhara alioufanya Kiembesamaki,
sehemu kubwa ya hotuba yake ililenga kuwahamasisha na kuwachochea vijana
wa chama chake kujiandaa kwa vurugu na kutotii sheria za nchi.
“UVCCM
tunaamini vitendo hivyo viovu na vya kikatili vilivyofanyika ni matokeo
ya matamshi ya uchochezi yaliyotolewa na katibu mkuu huyo na kuonyesha
ni chimbuko la kuanza kushamiri matukio ya uvunjaji wa sheria kabla ya
kufanyika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu,” alisema.
Alisema mara kadhaa UVCCM imekuwa
ikihimiza na kuwataka viongozi wa juu wa kisiasa kuchunga ndimi zao ili
kuendesha siasa za kuvumiliana, kushindana kwa nguvu ya hoja, pia
kuyaenzi na kuyalinda maridhiano ya kisasa yaliyofikiwa kati ya vyama
vya CCM na CUF hadi kuundwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa mwaka 2010.
“Inashangaza
hivi leo kumuona mmoja kati ya viongozi wanaojinasibu ni muumini na
waasisi wa maridhiano akipanda majukwaani na kuanza kurejesha siasa za
“mti kwa macho” na kushupaliana huku akitoa semi za uvunjaji wa
sheria, akisema yuko tayari hata kupigwa mabomu na kuwa wa kwanza
kuuawa hali inayoonyesha anakumbatia uvunjaji wa sheria,” alisema Shaka katika taarifa yake.
Chama cha CUF kimesema kutokea kwa
vurugu kisiwani Unguja juzi, kumesababishwa na kauli iliyotolewa na
Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Idd.
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa chama
hicho, Salum Bimani, alisema dalili za kutokea kwa vurugu na watu
kujeruhiwa zilianza muda mrefu.
HABARILEO
Polisi mkoani Katavi inamshikilia mkazi wa kitongoji cha Ntumba, kijiji cha Mnyengele wilayani Mpanda, Deogratius Pastory (30) kwa kumjeruhi vibaya mkewe kwa kumkata mkono wake wa kushoto na kupasua tumbo la mpenzi wa mkewe kwa panga.
Mtu huyo aliwatendea unyama huo baada ya kuwafumania mkewe aitwae Tabu Nestory (20) na mpenzi wake wa kiume aitwaye Masaga Elias (28) wakifanya mapenzi katika jiko la nyumbani kwake kijijini humo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari alithibitisha mkasa huo.
Alisema tukio hilo ni la Machi 23, mwaka
huu saa tano usiku katika kitongoji cha Ntumba katika kijiji cha
Mnyengele. Akielezea mkasa huo, Kidavashari alidai kuwa jioni ya siku
hiyo ya tukio, mtuhumiwa alimuaga mkewe Tabu kuwa anakwenda kijiji
ambacho kiko umbali mrefu kutoka kijijini hapo kwa ajili ya kuangalia
shamba lao.
Inadaiwa mtuhumiwa huyo alitumia
baiskeli yake katika safari yake hiyo. Kwa mujibu wa Kamanda
Kidavashari, wakati mtuhumiwa huyo akiendelea na safari yake ghafla
baiskeli yake aliyokuwa akiitumia katika safari yake hiyo iliharibika,
wakati huo ilikuwa tayari imetimu saa tatu usiku .
“Kwa
sababu alikuwa bado amebakiza mwendo mrefu kufika alikokuwa akienda
aliamua kugeuza na kuanza kurejea nyumbani kwake, ambako alifika saa
tano usiku …na alipofika kwake alimkuta mkewe na mpenzi wake wakifanya
mapenzi katika jiko nyumbani kwake,” alieleza.
Inadaiwa kuwa kitendo hicho
kilimkasirisha mtuhumiwa, ambaye alimwamuru mkewe na mgoni wake kuingia
ndani, ambapo alimkamata mwanamume huyo na kumfunga kamba mikononi,
kisha akachukua panga na kumchana tumbo chini ya kitovu hadi utumbo wake
‘ukamwagika’ nje .
Kwa mujibu wa Kamanda Kidavashari, mtu
huyo alitumia panga hilo alilotumia kuchana tumbo la mgoni wake, kukata
mkono wa kushoto wa mke wake.
HABARILEO
Wazazi 19 wa wanafunzi walioshindwa
kuripoti kidato cha kwanza kwa mwaka wa masomo wa 2014/2015 wamehukumiwa
kifungo cha nje cha miezi mitatu kila mmoja kutokana na kosa la
kushindwa kuwapeleka watoto wao shuleni.
Wazazi waliohukumiwa kifungo hiki ni
wale wa kata za Mpindimbi na Lukuledi zilizopo katika Halmashauri ya
wilaya ya Masasi, Mtwara Aidha, wametakiwa kuripoti kwenye Mahakama ya
Mwanzo ya Lisekese wilayani hapa kila baada ya wiki mbili wakati wote
watakapokuwa wanatumikia adhabu yao.
Mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo ya Lisekese wilayani Masasi, Gloria Mkwera karani wa mahakama hiyo, Agnes Hanga
alidai washitakiwa hao walitenda kosa hilo mwanzoni mwa mwaka huu kwa
waliposhindwa kutimiza wajibu wao wa kuwapeleka watoto wao shuleni huku
wakijua ni wajibu wao.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment