Hii ndio rekodi iliyovunjwa na mtoto wa miaka miwili India
Mara
nyingi wazazi hushauriwa kuona umuhimu wa kukuza vipaji vya watoto wao
tangu wakiwa wadogo, taarifa ikufikie kuwa mtoto mwenye umri wa miaka
miwili ameweka rekodi nchini India kutokana na uwezo wake wa kulenga
shabaha ya mishale.
Kutokana na vitabu vya kumbukumbu vya rekodi za taifa hilo, mtoto huyo Dolly Shivani Cherukuri, ameweka rekodi ya kuwa mshiriki mwenye umri mdogo zaidi kupata alama 200, katika mashindano yaliyofanyika wiki iliyopita.
Jarida la Press Trust
la India, limesema mtoto huyo alirusha mishale 36 kutoka umbali wa mita
5 na mita 7 na kupata alama 388, tukio lililoshuhudiwa na wachezaji
wakongwe na maafisa kutoka idara ya kumbukumbu za michezo.
Baba yake Cherukuri Satyanarayana ambae
ni mmiliki wa club moja inayofundisha kurusha mishale amesema,
alimfundisha kurusha mishale tangu alipozaliwa, kwa sasa ana mpango wa
kumpeleka kushiriki katika mashindano ili afikie hatua ya kuingia kwenye
kitabu cha rekodi za dunia cha Guinness.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment