Gazeti la Sweden limezileta hizi mpya za Zlatan Ibrahimovic!

Wino umekolezwa baada ya kuandika kwamba
staa huyu ameomba kibali cha kuishi na kufanya kazi nchini Marekani,
yani hajaomba visa ya Utalii, anataka kukaa kwa Obama kabisa.
Gazeti limesema Zlatan alikwenda kwenye
ubalozi wa Marekani nchini Ufaransa ambapo pia gazeti hili limerudisha
nyuma kumbukumbu za Interview za Zlatan ambae aliwahi kusema anapenda
kwenda kucheza soka la Marekani na akamtolea mfano Thiery Henry wakati
huo.
Zlatan ambae mkataba wake na PSG ya Ufaransa una uhai mpaka 2016, alisema pia ‘Ni kitu poa sana… na kama nafasi itatokea au kama bado ipo ndani ya miaka miwili au mitatu nitashawishika’
Habari hii imeripotiwa pia na mlssoccer.com pamoja na Sky Sports.
No comments:
Post a Comment