50 Cent kwenye headlines tena, safari hii anatafuta mpangaji..!
Msanii wa hip hop Marekani 50 Cent amekuwa akiingia kwenye headlines mbalimbali mara baada ya kutangaza kuwa amefilisika.
Headlines juu yake zinazidi kukua kila siku na safari hii headlines zinazomhusu 50 Cent ni za yeye kutafuta mpangaji wa nyumba yake ya Connecticut iliyopo Marekani.
Taarifa hizi zilianza kusambaa kwa fujo siku ya jumatano baada ya kukamilisha mkutano wake na Wanasheria.
Mwanasheria wa 50 Cent, Stephen Savva alisema japo hakuna mkataba wa upangishaji uliofikiwa kupangisha nyumba yake ya Farmington Mansion amabayo 50 aliinunua mwaka 2003…wamekuwa wakifanya mipango ya kupangisha nusu ya nyumba hiyo yenye vyumba 21, majiko 9 na casino lakini mpaka sasa rappa huyo hajabahatika kupata mpangaji.
Bado hatujasikia kiasi cha pesa ambacho
msanii huyo atatoza kama kodi ya nyumba, ila documents zilizowasilishwa
Mahakamani zinasema kuwa 50 Cent amekuwa akilipa dola 72,000 (Tzs.Milioni 144) kwa mwezi tu kama hela ya matunzo ya nyumba hiyo ambayo ni tofauti na kodi yake ya nyumba!
Duh! Unadhani hapa 50 Cent atapata mpangaji kweli kama pesa hii ni hela ya matunzo tu ya nyumba hiyo!?
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment