Kutana na uwanja huu wa mpira wa miguu unaobadilika rangi
Ujerumani ni moja kati
ya nchi zinazofanya vizuri katika dunia ya soka lakini pia iliwahi
kuandaa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2006… Sifa ya nchi hiyo sio tu
kuandaa michuano mikubwa bali hata kuwa na viwanja vizuri kama Olympiastadion na Allianz Arena.
Allianz Arena ni uwanja wenye muonekano kama puto kwa nje na unauwezo wa kuingiza watu 69,901, una uwezo kuingiza watu wengi zaidi ya Uwanja wa Taifa Dar Es Salaam
ambao unauwezo wa kuingiza watu 60,000 pekee. Umejengwa kwa euro
milioni 340, uwanja huo ni miongoni mwa viwanja vilivyotumika katika
michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2006.
Uwanja huu ambao upo mjini Munich Ujerumani hutumiwa kama uwanja wa nyumbani na vilabu vitatu vya mji huo, kama FC Bayern Munchen na TSV 1860 Munchen lakini kwa wakati mwingine hutumiwa na timu ya taifa ya Ujerumani,umekua pia kama kivutio
kizuri kwa mashabiki wanaokwenda uwanjani hapo kutazama mechi kwani
huwa unabadilika rangi kulingana na timu mwenyeji kwa siku hiyo atakuwa
nani.
Nimekusogezea pichaz na video za uwanja huo unavyobadilika rangi mtu wangu.
Ungana nami kwa habari, matukio na michezo hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment