Na hii ya mwanaume kusambaza ugonjwa kwa makusudi isikupite mtu wangu!
Nimekutana na stori kutoka Iceland inayomhusu mwanaume mmoja kutoka Nigeria ambaye amekamatwa na polisi kwa madai ya kusambaza ugonjwa wa UKIMWI kwa makusudi.
Mwanaume huyo ambaye jina lake bado halijajulikana ni raia kutoka Nigeria ambaye amekuwa akijaribu kupata uraia wa sehemu hiyo toka mwaka 2014.
Kwa mujibu wa ripoti kutoka kituo cha police cha Iceland, Iceland Review Report imesema:
>>>“sehemu
kubwa ya upelelezi tunaoufanya sasa hivi ni kujua kama wanawake wengine
wamekutana kimwili na huyu mwanaume zaidi ya ile idadi tulionayo kwenye
ripoti zetu…”<<< Iceland Police.
>>>“taarifa
zingine za matukio ya kiualifu ya mwanaume huyu bado zinakusanywa. Kwa
sasa shitaka kubwa dhidi yake ni kujihusisha na vitendo vya kimapenzi
kwa nia ya kusambabza ugonjwa wa UKIMWI- kitendo ambacho kikithibitishwa
kitakuwa ni kinyume na sheria zetu za nchi”. <<< Iceland Police.
Ungana nami kwa habari, matukio na michezo hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment