Arsenal yapata pigo.
Mkosi umezii kumuandama kiungo wa Arsenal Jack Wilshire ambaye taarifa toka jijini London zimearifu hii leo kuwa atalazimika kukaa nje ya uwanja kwa muda wa miezi zaidi ya miwili akiuguza jeraha sugu la kifundo cha mguu ambalo amekuwa nalo kwa muda mrefu .
Wilshere ameumia kwenye jeraha ambalo limewahi kumuweka nje ya jwanja kwa zaidi ya miezi sita na jeraha hili limeanza kuzua hofu ya kufupisha maisha ya soka la kulipwa kwa mchezaji huyu .
Wilshere ndiyo kwanza alikuwa anarudi uwanjani kwa mara ya kwanza baada ya kuumia mwanzoni mwa mwaka huu na mwezi mei na alianza kuonyesha ishara za kiwango ambacho kiliwafanya wengi kumtazama kama Gazza wa kizazi hiki .
Taarifa zaidi zinasema kuwa kiungo huyu anaweza kuwa nje kwa muda mrefu zaidi endapo itagundulika kuwa jeraha lake linahitaji kufanyiwa upasuaji na atafanyiwa vipimo zaidi ambavyo vitaonyesha ukubwa wa jeraha hilo mwishoni mwa wiki hii .
Historia ya Majeraha ya Wilshere.
Oktoba 2009 – Enka (Nje wiki 5)
Januari 2010 – Msuli wa Paja (Wiki 5)
Novemba 2010 – Mgongo (Wiki 2)
Agosti 2011 – Enka (Miezi 14)
Februari 2013 – Paja (Wiki 1)
Machi 2013 – Enka (Wiki 4)
Mei 2013 – Enka (Wiki 7)
Oktoba 2013 – Enka (Wiki 2)
Januari 2014 – Enka (Wiki 2)
Machi 2014 – Enka (Wiki 8)
Oktoba 2014 – Enka (Wiki 2)
Novembea 2014 – Enka (Miezi 5)
Agosti 2015 – Enka (Miezi 2)
No comments:
Post a Comment