Mfanyabiashara wa matunda mji mdogo wa Mombo Mkoani Tanga, Abubakary Ramadhani, akipanga bidhaa
zake kusubiri wateja. Wafanyabiashara hao wamekuwa wakilalamika kukosa soko la
uhakika la kuuzia bidhaa zao na balada yake hutegemea wasafiri wa mabasi
yaendayo Mikoani na kuwauzia kwa bei ya
kutupa ili kuepuka kuwaozea mikononi.
Kwa muda mrefu wafanyabiashara hao wamekuwa wakilalamika kukosa soko jambo ambalo limekuwa likiwapunguzia kasi ya kilimo hicho na kubadili aina ya kilimo.
Kwa upande wa Serikali imekuwa ikitoa ahadi kemkem na kuwatia matumaini ambapo viongozi wa Serikali imekuwa ikifanya jitihada za kuwatembelea mashambani na kutoa hofu ya ahadi zake.
Wadau mbalimbali wa kilimo na matunda wamekuwa wakifanya jitihada za kuliokoa zaio la matunda Wilayani Korogwe na Lushoto zikiwemo Asasi mbalimbali zikiwemo Oxfam na MUVI.
Hiii imekuwa iwaleta faraja na kutarajia siku moja kiwanda cha kusindika matunda kitajengwa Wilayani humo na kuondokana na umasikini na kuweza kuwa wakulima wakubwa na wa kisasa
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment