Hadithi hii inaletwa kwenu kwa hisani kubwa na Mkombozi Sanitarium Clinic, Mabingwa wa magonjwa sugu na yaliyoshindikana. Mkombozi wako na mashine za kisasa za kugundua magonjwa mwili mzima na kutoa tiba ya uhakika. Mkombozi ni kituo cha kisasa chenye Madaktari waliobobea. Kituo kipo Tanga mtaa wa Chuda mkabala na Kampuni ya mabasi ya Raha Leo, simu 0654 361333
ILIPOISHIA
“Ni mambo yangu binafsi”
“Kwa hiyo huna tatizo
jingine?’
Msichana akabetua mabega.
“Mimi sina tatizo, ni
wasiwasi wako tu”
Nikamsogelea karibu na
kumuuliza.
“Hivyo vitu umevizika kwenye
kaburi gani?”
Akanionesha kaburi lililokuwa
upande wa pili pembeni mwa ule mti.
Wakati nalitazama hilo kaburi aliniuliza.
SASA ENDELEA
“Je wewe mwenzangu ulikuwa
unafanyaje?”
“Kwani hukuniona?’
“Wakati ninakuja hapa,
nilikukuta unafukia lile kaburi”
“Mimi pia nilizika vitu
nilivyopewa na mganga” nikamdanganya.
“Mbona umetumia shepe?”
“Kwani wewe umechimba na
nini?”
“Kwa mkono, shimo dogo tu”
“Mimi nilizika vitu vingi,
ilibidi nifukue kwa shepe”
“Sawa. Nimekuelewa”
“Kwanini ulivua nguo?”
“Ndivyo nilivyoagizwa na
mganga”
“Kweli kila uganga una namna
zake”
“Haya mimi naenda zangu”
Sikupenda kuachana na yule
msichana mara moja, nikamuuliza.
“Unaishi wapi?”
“Ninaishi Mabawa”
Eneo alilolitaja ni jirani na
eneo la Msambweni.
“Mimi nimeshamaliza, twende
nikupeleke”
“Nitashukuru sana kakangu”
Tukaenda kwenye teksi,
nikaliweka shepe pamoja na tochi nyuma ya boneti kisha tukajipakia. Niliiwasha
teksi nikarudi kinyumenyume bila kuwasha taa.
Nilipotokea barabarani
nikawasha taa za teksi na kukanyaga mafuta.
“Unaishi sehemu gani?”
nikamuuliza yule msichana wakati teksi ikiwa katika mwendo.
Akanielekeza mtaa aliokuwa
anaishi.
“Unafanya kazi au upo
nyumbani?” nikamuuliza.
“Nafanya biashara zangu tu”
Sikumuuliza kitu tena hadi
nilipomfikisha nyumbani kwake. Nilimuacha anabisha mlango, nikaondoka. Kusema
kweli alikuwa msichana asiye na uoga. Usiku kama ule aliweza kwenda makaburini
akiwa pake yake akavua nguo na kuzika vitu kwenye kaburi! Nilimsifu kimoyomoyo
kuwa alikuwa jasiri.
Wakati ninarudi nyumbani
nilipanga kutomuelezea mtu yeyote kuhusu kifo cha mke wangu.
Nilijiambia mtu yeyote
atakayeniuliza nimwambie kuwa Halima amekwenda Pongwe kuwasalimia wazazi wake.
Zikipita siku tatu na mimi niende Pongwe, nizuge kwamba nimemfuata Halima.
Nitakapomkosa niende polisi kuripoti kuwa mke wangu amenitoroka.
Dakika chache baadaye
nikawasili nyumbani kwangu na kupatwa na mshituko nilipokuta mlango wa nyumbani
uko wazi. Nikajiuliza kama nilisahau kuufunga wakati nilipoondoka.
Nikashuka kwenye teksi na
kupiga hatua kuelekea mlangoni. Nilipoufikia mlango huo nilisikia hatua za mtu
akitembea humo ndani.
Nikajiuliza ni nani
aliyeingia ndani ya nyumba yangu, mwenyewe nikiwa sipo? Kitendo hicho kilikuwa
kimenishitua na kunipa taharuki lakini nilijikaza kiume. Kwa vile ilikuwa ni
nyumba yangu nikaingia.
Nikasimama kwenye sebule na
kuuliza kwa sauti ya juu.
“Nani ameingia humu ndani?”
“Shemeji!” nikasikia sauti ya
mwanamke ikitokea uani. Kisha nikamuona mwanamke mwenyewe. Kwa vile nilikuwa
nimesimama usawa wa mlango wa uani, na yeye aliniona.
“Shemeji! Akatamka tena huku
akinifuata.
Nilipomtazama vizuri nikamgundua.
Alikuwa ni Rita, dada yake marehemu mke wangu. Udugu wao ulikuwa ni wa shangazi
kwa mjomba.
Nilipooana na Halima yeye
ndiye aliyekuwa mstari wa mbele kusimamia harusi yetu.
“Oh kumbe ni wewe shemeji!”
nikamwambia na kumuuliza “Umekuja saa ngapi?”
“Nimekuja sasa hivi, nikakuta
mlango upo wazi. Naingia ndani sikuti mtu”
“Ah nilikuwa nimetoka mara
moja, nilisahau kufunga mlango”
“Huogopi waizi?”
“Nilisahau tu, si unajua
mambo ni mengi kichwani”
“Eh shauri yenu, mtakuja lia
kilio cha m’bwa!. Yuko wapi mwenzako?”
ITAENDELEA kesho na usikose nini kitajiri hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment