Man United imekubali kubadili jezi kwa kiasi hiki cha Pesa
Baada ya miaka 13 ya matumizi ya jezi za Nike kwa klabu ya Manchester United sasa imeamua kuzindua jezi mpya zitakazotumika katika msimu wa 2015/2016. Man United watatumia jezi zitakazokuwa zinatengenezwa na kampuni ya vifaa vya michezo ya ADIDAS kutoka Ujerumani.
Man United wamesaini mkataba wa miaka 10 na kampuni ya vifaa vya michezo ya ADIDAS, mkataba wenye thamani ya pound milioni 750 na sasa wataanza kutumia jezi za kampuni hiyo.
Ungana nami kwa habari, matukio na michezo hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment