Pep Guardiola ‘ngumi’ mkononi.
Makocha wa timu za barani ulaya hivi karibuni wamekuwa wakitengeneza vichwa vya habari hususan nchini England ambako Jose Mourinho na Arsene Wenger wamekuwa wakizungmzwa sana baada ya tukio la jumapili ambapo walichuniana .
Kocha wa Bayern Munich Pep Guardiola naye ameingia kwenye orodha hiyo baada ya kuingia kwenye ubishi mkali na kiungo wa Ac Milan Nigel De Jong wakati timu zao zilipokutana kwenye nusu fainali ya kombe la Audi.
Pep Guardiola ndio alianzisha ugomvi huo baada ya kuonekana amekerwa na kitendo cha De Jong kumchezea rafu kiungo wa Bayern Munich Joshua Kimmich .
Guardiola alikerwa na rafu ambayo aliicheza De Jong ambayo ilimsababishia kiungo huyo maumivu kiasi cha kumfanya atolewe uwanjani akishindwa kuendelea na mchezo huo .
Guardiola alimfuata De Jong wakati wa mapumziko na kuanza kumrushia kiungo huyo mdachi maneno makali hali iliyolazimu wachezaji wengine kuingilia kati kabla ugomvi huo haujawa mkubwa zaidi .
De Jong naye alijibu mapigo na kuzua tafrani kubwa na wachezaji wa Ac Milan walipata kazi ya ziada kumzuia kiungo huyo asiende kupigana na kocha wa Bayern .
Mchezo kati ya Ac Milan na Bayern Munich uliisha kwa Bayern kupata ushindi na kufuzu hatua ya fainali ambako watakutana na Real Madrid .
No comments:
Post a Comment