Utaratibu mpyampya ni huu, unapimwa uzito wewe na mizigo yako kabla ya kupanda Ndege !!
Ishu ya mizigo ya abiria kupimwa uzito kabla ya kupakiwa kwenye Ndege ni kawaida, mambo yamegeuka… Uzbekistan wanapima mpaka uzito wa abiria mtu wangu!!
Shirika la Ndege la Uzbekistan
limezigonga tena headlines kubwa duniani baada ya Shirika hilo
kutangaza kwamba wanaleta utaratibu ambao na abiria nao itabidi wapimwe
uzito kabla ya kupanda ndege, na hii sio kwa maana mbaya… wanaamua
kufanya hivi kama hatua ya kuchukua tahadhari kabla ya kuanza safari ili
wajue kabisa uzito ambao umepakiwa kwenye ndege.
Wamesema uzito wa mtu itakuwa ni taarifa
ya siri ambayo ni kwa ajili tu ya usalama wa Ndege zao kwenye safari,
hautaoneshwa mahali popote, japo hawajasema watafanya nini ikitokea
uzito wa abiria na mizigo utazidi kwenye kiwango kinachotakiwa kwenye
Ndege.
Nimejaribu kucheki mitandaoni na kukuta kumbe hii ya Uzbekistan sio mpya.. Samoa Air
ni Shirika le Ndege lililopo nchi ya Samoa, waliwahi kuutumia utaratibu
wa kupima uzito abiria ambapo ikitokea mtu amezidi uzito anatozwa bei
sawasawa na bei ambayo anatozwa abiria akizidisha uzito wa mzigo… na
malipo hayo ni nje kabisa ya nauli ambayo umeilipia.
Unaambiwa kwenye Ndege za Samoa Air waliweka mpaka siti za watu waliozidi uzito wa Kilo 130 ambazo zilipewa jina la ‘Samoa XL’, siti pana zaidi kuliko nyingine za kawaida.
Kwa habari , matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment