Monday, January 25, 2016

CUF KUTOFANYA MAADHIMISHO YA KUMBUKUMBU

Uchaguzi wa marudio Z'bar waivuruga CUF

Uchaguzi wa marudio wa Zanzibar ambao umepangwa kufanyika Machi 20, mwaka huu, umesababisha Chama cha wananchi (CUF) kushindwa kufanya maadhimisho ya kuwakumbuka wenzao waliofariki dunia mwaka 2001.

Maadhimisho hayo hufanyika Januari 27 ya kila mwaka yakishirikisha viongozi wakuu wa chama hicho pamoja na wafuasi wake.

  Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa chama hicho Taifa, Abdul Kambaya, alisema uongozi wa CUF taifa hautafanya maadhimisho hayo kwa kuwa siku hiyo Kamati Tendaji itakuwa inafanya kikao cha kujadili tarehe ya marudio ya uchaguzi ambayo ilitangazwa hivi karibuni na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (Zec).

Kambaya alisema siku hiyo kamati itakutana kuandaa ajenda kuhusiana na kutangazwa kwa tarehe hiyo ya uchaguzi ambazo zitapelekwa katika Baraza Kuu la chama.

Maandamano hayo yamekuwa yakifanyika kila mwaka kama kumbukumbu ya kuomboleza vifo vya wafuasi wa chama hicho waliouawa Januari 27, mwaka 2001 wakati wa maandamano ya kupinga matokeo ya urais visiwani humo.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment