Wednesday, January 13, 2016

DIWANI WA MAWENI ASEMA MIPANGOMIJI TANGA KUNA MATAMBAZI NA SIO MAJIPU



Tangakumekuchablog
Tanga, DIWANI kata ya Maweni halmashauri ya jiji la Tanga , Joseph Colvas (CCM), amemtaka Waziri wa Ardhi Nyumba na Makaazi, William Lukuvi, kufanya ziara Tanga na kuyatumbua majipu Idara ya mipangomiji kwa madai kuwa inagombanisha wananchi.
Akizungumza katika mkutano wa wananchi vijiji vinne Kange, Kasera, Kichangani na Saruji jana, Colvas alisema Idara ya hiyo  imejaa vishoka kwani imekuwa ikiwagombanisha wananchi kwa kuwapimia viwanja  na kuvigawa kwa wengine.
Alisema vishoka hao wamekuwa kero kwani wananchi wamekuwa hawafanyi kazi za kujiletea maendeleo na badala yake wamekuwa wakipanga foleni katika ofisi za mipangomiji na mwishoe hugombana wenyewe kwa wenyewe.
“Vijiji vyetu vimekuwa vikingia katika mgogoro usio wa lazima na hii inatokana na idara yetu yenye dhamana kuwalea vishoka, tunamuomba waziri mwenye dhamama kuja na kuyatumbua majipu” alisema Colvas na kuongeza
“Nawaomba ndugu zangu wananchi tuwe watulivu na tusigombane wenyewe kwa wenyewe tunajua pale mipangomiji kuna majipu yanataka kutumbuliwa na karibuni kazi itafanyika” alisema
Kwa upande wake mjumbe wa kamati ya mgogoro viwanja vya Kange, Suleiman Bindo, alisema kuna mapapa wanaowauzia watajiri viwanja vya wanyonge hivyo kuitaka Serikali kuwashughulikia.
Alisema wanawanchi wengi wameshindwa kuendeleza viwanja vyao na badala yake wamekuwa wakishinda mahakamani na ofisi za mipango miji jambo ambalo limekuwa likirudisha nyuma maendeleo.
“Viwanja vyetu vimekuwa vikiporwa kwa vile tuwanyonge hatuna uwezo wa kwenda katika ngazi za juu, tumechoka tumechoka kunyanyaswa na viwanja vyetu “ alisema
Ili kuweza kumaliza kero za viwanja halmashauri ya jiji la Tanga viongozi wa kata na Serikali za mitaa kata ya Mawezi kwa pamoja wamemtaka Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makaazi, William Lukuvi kwenda Tanga kupasua majipu.
                                         Mwisho



 Mkazi wa Saruji Kichangani halmashauri ya jiji la Tanga, Shaban Omari, akilalamika mgogoro wa ardhi kuongzeka eneo lao huku viongozi wenye dhamana wakilifumbia macho na kuwasababishia wananchi kugombana na kazi za kujitafutia maendeleo kusimama.

 Mkazi wa Kichangani kata ya Kange Tanga, Jumanne Salim, akizungumza kwenye mkutano wa wananchi uliokuwa ukizingumzia kuongezeka kwa migogoro ya ardhi eneo lao linalofanywa na vishoka na kusababisha wananchi kugombana.
  Mkazi wa Kange Kasera halmashauri ya jiji la Tanga, Ali Bakari Mdoe  akilalamika kuendelea  kuongezeka kwa migogoro ya ardhi eneo lao wakati wa mkutano wa wananchi  uliowashirikisha wananchi na viongozi wao wa Serikali za mitaa Kange, Kasera, Kichangani na Saruji.

No comments:

Post a Comment