Wednesday, January 13, 2016

RUNGU LAMUANGUKIA MWENGINE FIFA

Katibu wa FIFA naye kaungana na Sepp Blatter pamoja na Michael Platin kufungiwa..

Katibu mkuu wa Shirikisho la soka duniani Fifa aliyekuwa amesimamishwa kazi Jerome Valcke ameondolewa rasmi kutoka kwenye wadhifa huo na shirikisho hilo.
Mfaransa huyo, kwa sasa amesimamishwa kujihusisha na shughuli zozote za soka baada ya kudaiwa kuhusika katika njama za mauzo ya tiketi za Kombe la Dunia.
Maamuzi ya Fifa yamependekeza apigwe marufuku kuhusika katika shughuli zozote za soka kwa miaka tisa licha ya mwenyewe kukanusha madai hayo.
Valke ataunga na viongozi wengine wa FIFA baada ya Desemba mwaka jana Rais wa FIFA Sepp Blatter na rais wa UEFA Michel Platini, kufungiwa kujihusisha na soka kwa miaka 8 kufuatia uchunguzi wa zaidi ya upotevu wa Euro milioni1.35.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment