Saturday, January 30, 2016

RAHA YA KUSAFIRI ANGANI NA NDEGE UKIWA PEKE YAKO

Utajisikiaje siku unajikuta unasafiri pekeyako kwenye ndege kubwa? Imemkuta jamaa Ufilipino..

Inaweza kutokea unasafiri kwenye gari hivi labda toka Dar mpaka Morogoro kwenye basi la abiria pekeyako, unaweza kujifariji kwa kuchekicheki nje mazingira, ukachezea simu yako au ukaendelea zako na safari kwa kusikiliza muziki au kuangalia TV kwenye basi, kwenye ndege je inakuwaje?
Jamaa mmoja Alex Simon mtalii kutoka Austria, alijikuta kwenye level za kistaa hivi au mtu fulani VIP kwenye ubora wake baada ya kujikuta akiwa ndio abiria pekeake ndani ya ndege ya abiria zaidi ya 100… alitoka zake  Manila kwenda Boracay ndani ya Ufilipino kwa ajili ya kutalii tu !!
Baada ya Simon kuingia kwenye ndege alianza kupiga stori na marubani baadae akaungana na wahudumu wawili wa ndege wakiendelea na stori mpaka alipotua

Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment