Wednesday, January 27, 2016

VIMBWANGA VYA MASTAA UWANJANI

Hadi kufikia August 2014, hii ndio ilikuwa TOP 10 ya style mbaya za nywele kwa mastaa wa soka …

Kila staa kuweka style ya nywele katika muonekano tofauti tofauti, hususani katika muonekano ambao sio wa kawaida, yaani haujazoeleka machoni mwa watu. Hadi kufikia August 2014 hii ndio ilikuwa TOP 10 ya style mbaya za nywele kwa mastaa wa soka.
10- Raheem Sterling alikuwa katika hii list ila wakati huo akiwa katika klabu ya Liverpool ya Uingereza, Sterling kwa sasa anaichezea klabu ya Man City.
sterling_badhair
9- David James ni golikipa wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza na vilabu vya Liverpool na Manchester City, style yake ya nywele iliingia kwenye headlines hizi.
david-james-badhair-_58734a
8- Rene Higuita ni golikipa wa zamani wa timu ya taifa ya Colombia, ukiachana na style yake ya nywele kuwahi kuingia katika list ya style mbaya za nywele, anajulikana kwa style yake “scorpion kick” ya uokoaji mipira langoni.
higuita_badhair-600x415
7- Namba saba haikuwa ikimilikiwa na mchezaji mmoja, ila mabeki watatu  ndio walipata nafasi ya kumiliki namba ya count down hii, kutokana na style zao za nywele kufanana, David Luiz, Carles Puyol na Fabricio Coloccini.
3bad-hair
6- Marouane Fellaini style yake ya nywele haitofautiani sana na style ya nywele ya David Luiz, Carles Puyol na Fabricio Coloccini ila Fellaini kapewa namba sita. Fellaini anatajwa kuwa huenda umahiri wake wa kupiga sana mipira ya vichwa wakati akiwa Everton ulitokana na msaada wa nywele zake.
fellani_badhair-600x360
5- Ronaldo de Lima style yake ya nywele iliingia kwenye headlines katika fainali ya michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2002. Sababu ya Ronaldo kunyoa hivyo ni kutokana na mtoto wake kushindwa kuwatofautisha na Roberto Carlos wakati wanacheza mpira akiwaangalia kwenye TV.
ronaldo_badhair-600x600
4- Giovanni Simeone huyu ni mtoto wa kocha wa sasa wa Atletico Madrid Diego Simeone ambaye style yake ya nywele haikuishia kutajwa kuwa ni style mbaya pekee, ila inawezekana ikawa ni style mbaya kuwahi kutokea katika historia ya soka.
simeone_badhair
3- Djibril Cisse jamaa aliwahi kutamba na timu ya taifa ya Ufaransa na klabu ya Liverpool kati ya mwaka 2004 hadi mwaka 2007, Cisse amekuwa akijulikana kwa kupenda kubadili mitindo ya nywele kichwani, kitu ambacho kilimfanya pia kuwa maarufu ukiachana na uwezo wake uwanjani.
cisses_badhair
2- Chris Waddle kwa Uingereza hii ilikuwa moja kati ya style za nywele zilizowahi kuwekwa nakutamba licha ya kuwa zipo katika count down ya stori 10 mbaya, Waddle alikuwa kiweka mtindo huo wa nywele wakati akiwa Tottenham Hotspurs.
waddle_badhair
1- Taribo West katika count down hii huyu ndio staa pekee kutoka Afrika aliyeingia kwenye hii count down, staa huyo wa kimataifa wa Nigeria ambaye alistaafu kucheza soka miaka kadhaa nyuma, ndio alikuwa katika rekodi ya kuwa na style mbaya ya nywele kuliko wote.
west_badhair1
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment