Saturday, January 23, 2016

MAN U YACHECHEMEA

Hiki ni kipigo cha 6 cha Man United msimu huu, safari hii dhidi ya Southampton

Michezo ya Ligi Kuu Uingereza iliendelea jana  Jumamosi ya January 23 kwa michezo kadhaa kupigwa, mchezo wa kwanza uliyochezwa wa Ligi Kuu Uingereza ni mchezo kati ya Liverpool dhidi ya Norwich City, ulipigwa mapema kabla ya michezo mingine kuchezwa. Liverpool wakiwa ugenini walifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 5-4.
1453562526998_lc_galleryImage_MANCHESTER_ENGLAND_JANUAR
Baada ya hapo klabu ya Man United ambayo ilikuwa katika dimba lake la nyumbani Old Trafford, imekubali kipigo cha goli 1-0 kutoka kwa Southampton, Man United ambao bado kocha wao Louis van Gaal yupo katika wakati mgumu wa kuokoa kibarua chake, walishindwa kusawazisha goli hilo, baada ya kufungwa dakika za lala salama.
1453562252223_lc_galleryImage_Football_Soccer_Mancheste
Goli la Southampton lililofungwa dakika ya 87 ya mchezo na Charlie Austin limeifanya Man United kuendelea kuwa nafasi ya 5 katika msimamo wa Ligi, huku ikiwa na point 37 katika michezo 23, Huu ni mchezo 6 wa Man United wanapoteza toka kuanza kwa msimu wa 2015/2016.
Matokeo ya mechi nyingine za Uingereza zilizochezwa Jnuary 23
  • Norwich City 4 – 5 Liverpool
  • Crystal Palace 1 – 3 Tottenham Hotspur
  • Leicester City 3 – 0 Stoke City
  • Sunderland 1 – 1 AFC Bournemouth
  • Watford 2 – 1 Newcastle United
  • West Bromwich Albion 0 – 0 Aston Villa
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment