Monday, January 18, 2016

SIMBACHAWENE ATEMA CHECHE

Waziri Simbachawene kawasimamisha na hawa Wakurugenzi wengine…

Zoezi la kuendelea kuwatimua watendaji wasiowajibika katika ofisi za umma limeendelea kuchukua headlines kila siku..leo inawahusu wakurugenzi wa Manispaa za Kigoma, Katavi na Mpanda ambao wamesimamishwa kazi na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawene.
Uamuzi wa Mh.Simbachawene umekuja baada ya kubaini upotevu wa wa fedha za umma.
Taarifa iliyotolewa leo na Kitengo Cha Mawasiliano Ofisi ya Rais imesema Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Mhandisi Boniface Nyambele anakabiliwa na tuhuma ya uuzaji wa nyumba za Halmashauri bila kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo na bila kibali cha Waziri Mwenye Dhamana kama Sheria inavyo elekeza.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda Suleiman Lukanga ana kabiliwa na tuhuma za Ununuzi hewa wa gari la kusomba taka kwa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 90 na ubadhirifu wa fedha za ujenzi wa Skimu ya Umwagiliaji ya Kakese kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 200.
Mheshimiwa Waziri wa Nchi ameagiza nafasi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma ikaimiwe na Mhandisi Sultan Imari ambaye ni Mkuu wa Idara ya Maji, Manispaa ya Kigoma, nafasi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda ikaimiwe na Lauteri John ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi.
Pia amewataka  Wakurugenzi Watendaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kote Nchini kuwa makini katika kutekeleza majukumu yao wafuate  Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo kwani Serikali haitasita kuchukua hatua za kinidhamu kwa watumishi wote ambao watakiuka matakwa ya Sheria, Kanuni na Taratibu na kutoweka mbele maslahi ya Umma.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment