Monday, January 18, 2016

POLISI TANGA WAKAMATA BOTI TATU BANDARI BUBU ZIZLIZOSHEHENI MALI ZA MAMILIONI

 Polisi Mkoani Tanga kwa kushirikiana na kikosi cha Marine imekamata mashua tatu zinazoaminika kutoka Zanzibar zikiwa zimesheheni mali za magendo ya mamilioni ya fedha bandari bubu ya Kigombe nje kidogo ya jiji la Tanga.
Kukamatwa kwa maboti hayo imetokana na doria inayofanywa na kikosi cha Marine cha Tanga ambapo kwa muda mrefu Bandari hiyo imekuwa mwiba kwa polisi kwani wamekuwa wakipigwa chenga na wapitishaji mizigo ya magendo.
Hivi karibuni Polisi wakati wakiwa katika doria waliwafukuza wasafirishaji mali za magendo wanaotumia Pikipiki na gari yao kuserereka na dereva  kufa papo hapo na mwengine kufariki .
hospitali.
Kutoka hapo kikosi cha polisi cha mareni kimekuwa kikiongeza maradufu doria na kufanikiwa kuzikamata boti tatu leo zilizosheheni mali za mamilioni ya fedha.
Picha zita kiutoka ndani moja ya boti Kigombe Tanga







No comments:

Post a Comment