Tuesday, January 19, 2016

ALIEKUWA AKISHIKILIA UMRI MKUBWA DUNIANI AFARIKI

Mwanaume aliyeingia kwenye rekodi ya mtu mwenye umri mkubwa zaidi duniani…kilichonifikia leo ni hiki!.

on
Mwaka jana Yasutaro Koide aliingia kwenye kitabu cha kumbukumbu ya duniani cha Guiness baada ya kuwa mwanaume mwenye umri mkubwa zaidi duniani.
Mzee huyo alizaliwa Machi 13, 1903 katika jiji la Nagoya, Japan na amefariki leo akiwa na umri wa miaka 112 kutokana na maradhi ya moyo na nimonia.
Alichukua nafasi hiyo mwaka jana baada ya kifo cha bibi Misao Okawa kutoka Japan aliyefariki akiwa na umri wa miaka 117.
Alipoulizwa kuhusu siri ya maisha marefu wakati akiwa hai, alisema watu waache kufanya kazi ngumu na pia waishi kwa furaha.
Mpaka sasa bado haijafahamika nani atamrithi kama mwanamume mzee zaidi baada ya yeye kufariki. Kwa sasa mtu mkongwe zaidi duniani ni mwanamke Susannah Mushatt, raia wa Amerika ambaye ana umri wa miaka 116.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment