Monday, January 11, 2016

NSSF TAWI LA KOROGWE TANGA YAWAKUMBUKA WAGONGWA KILINDI



Tangakumekuchablog
Kilindi, MFUKO wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Tawi la Korogwe Mkoani Tanga limetoa msaada wa mashuka 100 kwa Zahanati ya Kwediboma Wilayani hapa kujikinga na baridi kwa wagongwa wanaolazwa kituoni hapo.
Akizungumza mara baada ya makabidhiano, Kaimu Meneja NSSF tawi la Korogwe,  Rebule Maira, alisema msaada huo ni moja ya misaada inayotoa kwa wateja wake vikiwemo vituo vya Afya na shule.
Alisema NSSF ilipata taarifa za  kituo  kukabiliwa na uhaba wa mashuka kwa wagonjwa wanaolazwa na hivyo mfuko kuona umuhimu wa kukisaidia na  kuweza kukabiliana na changamoto mbalimbali za wagonjwa.
Mfuko wa hifadhi ya jamii uko kwa ajili ya jamii na leo ndio maana tumekuja hapa kusaidia jamii, tumetoa mashuka kwa ajili ya wagonjwa kujikinga na baridi kali kama tujuavyo wilaya hii iko na baridi kali” alisema Rebule na kuongeza
“Mfuko uko na utaratibu wa kusaidia jamii ambapo hutenga fungu maalumu kama ujenzi wa maabara na shule pamoja na huduma nyenginezo niwahaakikishie wananchi lengo letu nikusaidia  jamii” alisema
Kwa upande wake mkuu wa kituo ambaye pia ni muuguzi kituo cha Zahanati Kwediboma, Sister Matilda Pitter, amesema kituo hicho kinakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo uhaba wa vitanda kwa wagonjwa na majengo.
Alisema kituo hicho kimekuwa kikipokea wagonjwa wengi na baadhi yao kutoka Handeni na Songe pamoja na vijijini hivyo kuyataka mashirika ya umma na Serikali kukisaidia na kuiga mfano wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF.
Alisema kituo kimekuwa kikipokea wagonjwa wengi tofauti na uwezo wake na hivyo kutaka kuongeza majengo ambayo yatakuwa na uwezo wa kupokea wagonjwa wengi wanalazwa.
“Zahanati yetu inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo uhaba wa majengo ambapo kwa sasa ndio kama unavyoona majengo tunayojenga , changamoto iko katika umaliziaji” alisema Matilda
Matilda ameitaka mifuko mengine  ya Hifadhi ya Jamii na mashirika na Serikali kukisaidia kituo hicho ili kuweza kuwapatia wananchi huduma ya matibabu na kuondosha kero ya kufuata matibabu masafa marefu.
                                         Mwisho



 Kaimu Meneja Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) tawi la Korogwe Tanga, Rebule Maira akimkabidhi mashuka 100 msimamizi wa Zahanati ya Kwediboma Wilayani Kilindi Mkoani Tanga, Sister Maltilda Pitter, ikiwa ni msaada kwa wagonjwa wanaolazwa kituoni hapo, wa tatu kutoka kulia ni Dr, Thomas Muyombo na mwisho kusoto ni Muuguzi wa zamu, Siwazuri Matata.



No comments:

Post a Comment