Tuesday, January 26, 2016

WENGER AIBUA NA KULIZWA

TOP 3 Stories: Pique katwaa tuzo mbele ya Messi, Real Madrid wameanza mazungumzo na Neymar, FC Barcelona wamewaharibia Arsenal …

Stori kubwa za siku katika michezo. Leo January 26 naomba nikusogezee TOP 3 stories kubwa.Real Madrid na Atletico Madrid wameshindwa kuibuka na ushindi katika michezo yao ya weekend na kuiacha FC Barcelona kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi ila hizi ni habari kubwa za siku kutoka Hispania.
3- FC Barcelona wana mipango ya kuivurugia Arsenal
Klabu ya FC Barcelona ya Hispania inaripotiwa kuwa na mipango ya kutaka kumsajili Nolito kutoka Celta Vigo, staa huyo pia alikuwa anawaniwa na Arsena kwa kiasi kikubwa hivyo mpango wa FC Barcelona kumuhitaji ni sawa na kuingilia mipango ya Arsenal. Tayari Rais wa Celta Vigo amemwambia kocha wa FC Barcelona atoe euro milioni 18 ili waweza kumpata staa huyo.
Nolitoz
2- Klabu ya Real Madrid imeanza mazungumzo na Neymar.
Klabu ya Real Madrid ya Hispania kwa mujibu wa stori kutoka Hispania wanaripotiwa kuanza mazungumzo yasio ya moja kwa moja na muwakilishi wa staa wa FC Barcelona Neymar, kwa mujibu wa ripota wa michezo Eduardo Inda anaripoti kuwa Real Madrid wapo tayari kutoa euro milioni 180 ili wanase saini ya Neymar.
Neymar-goal1 (1)
1- Gerrard Pique ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa FC Barcelona
Beki wa kati wa klabu ya FC Barcelona ya Hispania Gerrard Pique, ametangazwa kuwa mchezaji bora wa mwezi wa klabu ya FC Barcelona ya Hispania na kuwashinda Lionel Messi na Andrea Iniesta. Pique pia alitangazwa kuwa katika kikosi bora cha FIFA cha mwaka 2015.
Pique-
Kwa habari matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment