Saturday, January 23, 2016

MOURINHO AITAMANI LIGI KUU ENGLAND

Mourinho na barua nzito kwa klabu ya Man United..amesisitiza jambo!!

Jose Mourinho kwa sasa ni kocha huru..hii ni baada ya kufukuzwa katika klabu ya Chelsea baada ya kuonekana ikisuasua kwenye ligi kuu msimu huu.
Kocha huyo bado ameonekana kutamani kuzifundisha klabu za ligi kuu na sasa ameamua kuandika barua yenye kurasa sita kwa uongozi wa klabu ya Man United akizungumzia mipango yake mipya ya kuhakikisha anaiweka klabu hiyo kwenye nafasi nzuri.
Kusuasua kwa klabu ya Manchester United kwa sasa kunampa nafasi ndogo kocha wake wa sasa Van Gaal kuendelea kuitumika timu hiyo huku Mourinho akijipa matumaini makubwa huenda akapewa kibarua hicho baada ya kuondoka kwa kocha huyo.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment