Friday, January 8, 2016

KAMPUNI YA QUALITY MEDIA GROUP YALINUNUA GAZETI LA JAMBO LEO

Kama ulikuwa hujui gazeti la Jambo Leo limeuzwa, mipango mingine 2016 nimesogezewa pia..

Kampuni  ya Quality Media Group Limited imeinunua kampuni ya Jambo Concepts Tanzania Limited ambao ni wachapishaji wa gazeti la kila siku la Jambo Leo na ununuzi huo umeanza December 31 2015 na unatarajiwa kukamilika Februari 2016.
4Kampuni ya Quality Media imedhamiria kuwekeza katika tasnia ya habari kwa kuongeza ufanisi katika utendaji wa gazeti la Jambo Leo na kuahidi kufikia mwisho wa robo ya kwanza ya mwaka 2016 kuongeza machapisho mengine ikiwa ni pamoja na gazeti la kiingereza la kila siku na gazeti toleo la wiki la Afrika Mashariki.
2Mkurugenzi mtendaji wa Quality Group, Bw. Arif Sheikh amesema Kampuni ya Quality Group imejipanga kuhakikisha kuwa Jambo Media inakuwa chombo cha habari bora na cha kuaminika nchini Tanzania katika ukanda wote wa Afrika Mashariki.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment