Thursday, January 14, 2016

WAFANYABIASHARA KITUO CHA MABASI KOROGWE WALALAMIKA

 Wajasiriamali biashara ya matunda kituo cha mabasi Wilayani Korogwe Mkoani Tanga wakisubiri wateja, Wafanyabiashara hao  wamepewa siku tano kuondoka kituoni hapo kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kitisho cha kuzuka kwa ugonjwa wa kipindupindu, hata hivyo wamepinga amri hiyo na kusema kuwa ni njama za kuwadhoofisha kimaisha.
Hatua hiyo imepingwa vikali na wafanyabiashara hao na kusema kujiajiri kwao imekuwa nongwa na kudai kuwa mikopo waliokopa itawapeleka gerezani.
Wamesema ili kuweza kufanya biashara zao na kuweka mazingira mazuri maeneo yao ni vyema Serikali kuhamasisha usafi muda wote.




No comments:

Post a Comment