Wednesday, January 27, 2016

ADEBAYOR AIBUKIA CRYSTAL PALECE

Baada ya kutemwa na kocha wa Spurs hii ndio klabu aliyojiunga nayo Emmanuel Adebayor

Mshambuliaji wa kimataifa wa Togo aliyewahi kuvichezea vilabu vya Arsenal, Man City na baadae Tottenham Hotspurs Emmanuel Adebayor alikuwa hana timu kwa miezi kadhaa sasa, baada ya kocha wa klabu yake ya Tottenham Hotspurs Mauricio Pochettino kumuondoa katika mipango na kikosi chake kitakachoshiriki mashindano tofauti, licha ya kuwa alikuwa analipwa kama kawaida.
saaa
January 26 mitandao ya soka ya Uingereza imethibitisha Adebayor kujiunga na klabu ya Crystal Palace ya Uingereza,  Sky Sport wamethibitisha staa huyo kujiunga na klabu hiyo hadi mwishoni mwa msimu.
3099B64200000578-3417775-Adebayor_has_been_handed_the_No_25_shirt_by_the_club_and_will_be-m-27_1453830804947
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment