Friday, January 22, 2016

BABU MOURINHO AIBUKIA SIASA KWAO

Baada ya kufukuzwa Chelsea, Jose Mourinho kahamishia maneno yake kwenye siasa za Ureno …

Baada ya uongozi wa Chelsea kumfukuza kazi aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo Jose Mourinho na nafasi yake kuchukuliwa na Guus Hiddink kama kocha wa muda wa Chelsea, Mourinho ameingia kwenye headlines ya kampeni za kisiasa, mreno huyo ameingia kwenye headlines baada ya kutia neno katika siasa za nchini kwake.
Stori kutoka today.ng zinaeleza kuwa Jose Mourinho amewaomba wareno wenzake wasifanye makosa ya kumchagua kiongozi wamtakaye, lakini Jose Mourinho amewaomba wamchague Marcelo Rebelo de Sousa kama mtu sahihi wa kuwaongoza.
“Kwa mara ya kwanza ndio najitokeza kuonesha namuunga mkono mgombea gani, kwa sababu nafikiri huu ni wakati sahihi kwa Ureno kufanya chaguo sahihi, zaidi ya miaka ya nyuma” >>> Mourinho
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment