Monday, January 11, 2016

VIBIRU UKOCHA ULAYA

Kama Guardiola akijiunga na Man City, kocha wa Man City Manuel Pellegrini anatajwa kuamua hivi …

Ni siku kadhaa zimepita toka kocha wa klabu ya FC Bayern Munich ya Ujerumani Pep Guardiola atangaze kuwa hatoendelea kuifundisha FC Bayern Munich, baada ya msimu kumalizika, bali ataendelea kutafuta changamoto mpya sehemu nyingine ila sana ana husishwa kwenda kujiunga na klabu ya Man City ya Uingereza, kwani ndio nchi ambayo ana mpango wa kwenda kufanya kazi.
MANCHESTER, ENGLAND - NOVEMBER 25: Josep Guardiola the head coach of Bayern Muenchen gestures as Manuel Pellegrini the manager of Manchester City looks on during the UEFA Champions League Group E match between Manchester City and FC Bayern Muenchen at the Etihad Stadium on November 25, 2014 in Manchester, United Kingdom. (Photo by Laurence Griffiths/Bongarts/Getty Images)
Kocha wa sasa wa klabu ya Man City Manuel Pellegrini ambaye anatajwa kuwa katika wakati mgumu kuishawishi bodi ya klabu hiyo iendelee kumuamini, anatajwa kama nafasi yake ikichukuliwa na Pep Guardiola basi yeye huenda akaenda kujiunga na klabu ya Chelsea ya Uingereza ambayo nayo ina kocha wa muda baada ya kumfukuza Jose Mourinho.
adfghjks
Hii ni tweet ya ripota wa kituo cha Sky Sport ikielezea uwezekano wa Pep kusaini Man City na Manuel kujiunga na Chelsea
Kauli ya Pep Guardiola wakati akithibitisha kuwa hana mpango na FC Bayern Munich baada ya msimu kumalizika “Nina fursa ya kufanya kazi Uingereza, nafikiri nina umri sahihi na wakati sahihi wa mimi kwenda huko. Ni kweli nimepokea ofa kadhaa kutoka Uingereza lakini siwezi kuongelea zaidi kwa sababu sijasaini klabu yoyote”
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment