Thursday, January 21, 2016

BARAZA LA MJI WETE LAPIGA MARUFUKU ULAJI NA UUZAJI VYAKULA BARABARANI



Tangakumekuchablog

Pemba, BARAZA la mji Wilaya ya  Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba, Imepiga marufuku ulaji na uuzaji holela wa chakula barabarani na mitaani kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kujikinga na ugonjwa wa Kipindupindu uliopiga hodi mjini hapa.

Marufuku hiyo pia  imewalenga wenye hoteli na migahawa barabani ambapo wanalazika kuomba vibali maalumu vya biashara na kukaguliwa na baraza hilo kujiridhisha na mazingira ya eneo husika.

Hatua hiyo iliyochukuliwa na baraza la mji imelalamikiwa na wamiliki wa hoteli na migahawa barabarani na kusema kuwa  ni sheria kandamizia hivyo kulitaka kubatilisha na kuangalia njia mbadala.

Baadhi ya wamiliki wa migahawa waliozungumza na kituo hiki wamesema ugonjwa wa kipindupindu ni uchafu hivyo baraza la mji kutakiwa kusimamia zoezi la usafi lililoanzishwa na Rais Magufuli.

Wamesema hatua hiyo imeleta athari kwa wafanyakazi na wamiliki wa mahoteli jambo ambalo limewalazimu kuwapa likizo bila malipo wafanyakazi wao.

                                                     Mwisho

No comments:

Post a Comment