Tangakumekuchablog
Tanga, WAHITIMU Chuo Kikuu Huria (OUT)
tawi la Tanga, wametakiwa kuwa mabalozi wazuri wa kupiga vita rushwa maofisini na
badala yake kuwa wabunifu katika
utendaji kazi.
Akizungumza
wakati wa mahafali ya 31 Chuo Kikuu Huria (OUT) tawi la Tanga jana, Katibu
Tawala Mkoa wa Tanga, Zena Said, alisema kuna baadhi ya wakuu katika idara
hawatoi huduma bila kudai rushwa.
Alisema
tabia hiyo imekuwa ikirudisha nyuma maendeleo ya wananchi na kuamini kuwa
huduma haitolewi bila kutoa rushwa jambo ambalo sio sahihi na kuwataka kwenda
katika vituo vyao na kuwa mabalozi wema.
“Kupitia
mahafali haya natambua kuwa hapa kuna wahitimu wa fani mbalimbali zinazogusa
sekta nyeti ikiwemo ya polisi na utoaji wa huduma kwa jamii” alisema Zena na
kuongeza
“Kuna dhana
kwa baadhi ya watu kuamini kuwa huduma haitolewi bila kutoa rushwa, hii tunataka
kuikomesha na kufanya hivyo ni ninyi hapa kuwa mfano kwa wengine” alisema
Kwa upande
wao wahitimu wa mahafali hayo wameiomba Serikali kuongeza nafasi za ajira
Serikali ili kuepuka elimu yao kuishia mifukoni.
Walisema
kuna wimbi kubwa la watu wenye elimu lakini wamekosa nafasi za kazi hivyo
kupunguza kasi ya ufanisi wa utoaji huduma kwa jamii na nguvu kazi ya maendeleo
ya wananchi.
Mmoja wa wahitimu wa mahafali 31 Chuo Kikuu OUT tawi la Tanga akimuweka sawa mwanafunzi mwenzake kabla kwenda kutunukiwa cheti na mgeni rasmi Katibu Tawala Mkoa wa Tanga, Zena Said juzi.
No comments:
Post a Comment