Sunday, December 25, 2016

GEREZA KUU LA KIGALI RWANDA LATEKETEA KWA MOTO

Gereza kuu la Kigali lateketea kwa moto

Gereza kuu la Kigali maarufu 1930
Gereza kuu la Kigali maarufu 1930 lateketea kwa moto. kufikia leo jioni moshi inaendelea kutanda. Kilichosababisha moto huo hakikajulikana.
Shughuli za kuzima moto bado zinaendelea huku vikosi vya Askari Jeshi na polisi vikionekana hapa na pale kando kando mwa jengo la gereza hilo.
 Hilo Ni gereza linalohifadhi wafungwa wa mchanganyiko wale wa kisiasa na wengine wa mauaji ya kimbari. Miongoni mwa wafungwa wa kisiasa Ni Victoire Ingabire aliyehukumiwa kifungo cha miaka 15 jela miaka 4 iliyopita Kwa hatia ya kuchochea utengano wa kikabila na kuhatarisha usalama wa raia.
Viongozi kadhaa serikalini wamefika kwenye eneo la tukio wakiwemo mawaziri na wakuu wa jeshi na polisi.
Bado Ni mapema kujua athari zilizotokana na tukio hilo kwani waandishi wa habari hawajaruhusiwa kuingia katika jengo la gereza kuu ya Kigali.
Magari ya zima moto bado yanapishana na magari ya kubeba majeruhi huku wafungwa wakionekana nje ya gereza na ulinzi ukiwa umeimarishwa.
BBC

No comments:

Post a Comment