Sunday, December 25, 2016

PICHA 15 WALIOZALIWA MKESHA , IBADA HADI SHEREHE UOGELEAJI BEACH RASKAZONE, TANGA



Tanga, JAMII imetakiwa  kuwa na upendo kwa watu wanaoishi katika mazingira magumu  kwa kuwapa misaada pamoja na kutoa ushauri nasaha kwa watu ambao wameathirika na madawa ya kulevya.
Akiwahutubia waumini wa dini ya Kikristo wakati wa ibada ya Sikuu ya Krismass Kanisa la Glory Land Sabasaba Tanga Leo, Mchungaji wa kanisa hilo, Manasse Maganga, alisema jamii imejisahau hivyo kuwakumbusha kwa kuwakumbuka kundi hilo.
Alisema mbali ya Tanga kupungua kwa watumiaji wa madawa ya kulevya lakini iko haja ya kutoa elimu shuleni, vyuoni na mitaani ili kuokoa nguvu kazi ya Taifa la baadae.
“Siku ya leo ni siku adhimu na furaha kwa kila mmoja wetu tufuraahi na kula chakula kwa pamoja bila kubaguana kwa rangi wala kabila, sote tunatokana na Mungu mmoja” alisema Maganga na kuongeza
“Kwa mujibu wa takwimu Tanga inaonyesha watumiaji wa madawa ya kulevya imepungua, ila tusibweteke tupambane shuleni vyuoni hadi mitaani ionekane utumiaji wa madawa ya kulevya ni dhambi mbaya” alisema
Akizungumzia umoja amani na usalama wa nchi, Mchungaji huyo aliwataka wananchi kuitunza amani iliyopo kwani ikitoweka ni gharama kuirejesha tena.
Alisema inapaswa kuvumiliana na kila mmoja kujua wajibu wake na mipaka yake katika utendaji wa kazi lengo likiwa ni kuienzi amani na utulivu uliopo.
Alisema kwa mnasaba wa siku hiyo ya Krismass kila mmoja kushika neon amani uvulivu na upendo na kusema kuwa kufanya hivyo Tanzania itaendelea kuwa kisiwa cha amani na mataifa ya nje kuja kujifunza,.
                                               



Muuguzi wa zamu kituo cha Afya cha Ngamiani Tanga, Amina Mashaka, akimpa mtoto wake mzazi Nusra Hashim alijifungua mkesha wa Sikukuu ya Krismass leo.





Mchungaji wa Kanisa la Glorland la Sabasaba Tanga, Manase Maganga, akiwahutubia waumini wa kanisa lake wakati wa ibada ya Sikukuu ya Krismass leo . 

 Waumini wa Kanisa la Gloryland Sabasaba Tanga, wakiomba maombi kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli wakati wa ibada ya Sikukuu ya Krismass leo.






, Wakazi wa Tanga na maeneo ya jirani ya Mkoa huo  wakiogelea Beach ya Raskazone kusherehekea Sikukuu ya Krismass  leo..

No comments:

Post a Comment