Afisa mkuu wa NIMR aliyetangaza kuna Zika Tanzania afutwa kazi
Mkurugenzi wa
Taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu nchini Tanzania (NIMR), Dkt
Mwele Malecela, ambaye alitangaza kugunduliwa kwa virusi vya Zika nchini
Tanzania, amefutwa kazi.
Taarifa kutoka kwa mkurugenzi wa
mawasiliano ya ikulu Gerson Msigwa inasema Rais wa John Magufuli
ametengua uteuzi wa mkurugenzi huyo mkuu.Taarifa hiyo hata hivyo haijaeleza sababu ya kufutwa kazi kwa Dkt Malecela, siku moja tu baada yake kutangaza kwamba kuna virusi hiyo.
Hata hivyo, kulikuwa kumetokea habari za kukinzana kutoka kwake na wizara ya afya kuhusu kuwepo kwa virusi vya Zika nchini Tanzania.
Alitangaza kuwepo kwa virusi hivyo nchini Tanzania siku ya Alhamisi lakini Ijumaa, baada ya habari hizo kuenea kwenye vyombo vya habari, waziri wa afya Ummy Mwalimu akatoa taarifa kukanusha habari hizo.
BBC
No comments:
Post a Comment