Saturday, December 10, 2016

PEP GUARDIOLA AUNGA MKONO KUONGEZWA WACHEZAJI KOMBE LA DUNIA

Guardiola ataka wachezaji wa ziada kuongezwa

Kocha Pep Guardiola wa Manchester City ataka idadi ya wachezaji wa ziada kuongezwa hadi sita
Kocha wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola amesema kuwa Fifa inafaa kufikiria kuongeza wachezaji wa ziada na kufikia hadi sita ili kukabiliana na tishio la kuwachosha wachezaji.
Shirika la soka duniani Fifa wiki hii lilithibitisha kuwa litaongeza idadi ya timu zinazoshiriki katika kombe la dunia hadi 48 ikiwa na makundi 16 yenye timu tatu.
Guardiola amesema kwa hatua ya kuongeza idadi ya mechi zitakazochezwa itawachokesha wachezaji.
BBC

No comments:

Post a Comment