Tuesday, December 20, 2016

LIPULI ILIVYOIBAMIZA ARFICAN SPORTS NYUMBANI KWAO MKWAKWANI



Tangakumekuchablog
Tanga, KOCHA wa African Sports ya Tanga inayoshiriki ligi daraja la kwanza Tanzania Bara, Ali Bhai, amejitetea kipigo cha goli moja walichopewa na Lipuli kuwa wachezaji wake walikaba sana kulikoni kupiga mashuti.
Akizungumza mara baada ya dakika 90 ya kipenga cha mwisho wa mchezo uwanja wa Mkwakwani juzi , Bhai, alisema Lipuli walicheza pasi ndefu ambazo wacjhezaji wake ziliwachanganya.
Alisema mwazo wa mchezo aligungua uchezaji wa Lipuli kwa mfumo wao waliouanza alitambua kuwa mambo yatakuwa wagumu na kushindwa kujipanga.
‘Wenzetu dakika ya kwanza tu walianza kwa mipira mirefu ambavyo hatukutarajia, wakati wao wakiendeleza hayo tukabaki kukaba sana kulikoni kupiga mashuti” alisema Bhai na kuongeza
“Kwa kweli unapofungwa nyumbani ni aibu mbele ya washabiki wako ambao walikuwa wakikushangilia mwanzo mwisho, tunarejea kambini kupeana mbinu ya uchezaji endapo mpinzani wake amecheza mchezo ambao hukuutarajia” alisema
Kwa upande  wake kocha wa Lipuli, Lucac Kambanyino, amesema kupata pointi tatu ugenini ni fahari na kuwa na moyo wa kufanya vizuri kila mchezo ulioko mbele yako.
Alisema bao moja   walilolipata mwanzo mwa mchezo na kuwapa pointi tatu muhimu haikuwa rahisi kwani wenyeji wao walikuwa wakishangiliwa kwa nguvu jambo ambalo niliamini mambo yatakuwa magumu.
“Bao lile la mapema lilitusaidia na kuwachanganya wenyeji wetu kwani walikuwa wakikaba zaidi nasi tukaona ni bora kucheza pasi ndefu ambazo zilisaidia” alisema Kambanyino
Kocha huyo alisema wanarejea kwao Iringa kwa kuamini kuwa ligi hiyo iko na safari ndefu na changamoto nyingi za kutokuwa na udhamini  jambo ambalo timu zinazoshiriki kuwa katika wakati mgumu.
Wachezaji wa timu ya Lipuli wakijichanganya wakati wa mchezo wao na timu ya African Sports uwanja wa Mkwakwani ligi daraja la kwanza juzi, Lipuli ilishinda kwa bao 1.


  Mchezaji wa African Sports, Farid Said akimiliki mpira wakati wa mchezao ligi daraja la kwanza Tanzania Bara uwanja wa Mkwakwani dhidi ya Lipuli juzi, Lipuli ilishinda bao 1.
 Wachezaji wa African Sports wakimdhibiti mchezaji w alipuli wakati wa mchezo ligi daraja la kwanza Tanzania Bara uwanja wa Mkwakwani juzi, Lipuli ilishinda bao 1.
Mchezaji wa African Sports, Hamadi Faki akipifa Tiktaka kuelekeza mpira langoni kwa Lipuli wakati wa mchezo ligi daraja la kwanza Tanzania Bara uwanja wa Mkwakwani juzi, Lipuli ilishinda bao 1.

No comments:

Post a Comment