Taarifa ya Lori la mafuta lililolipuka Kenya na kusababisha vifo
Lori la mafuta limelipuka nje ya mji wa Naivasha nchini Kenya usiku wa Jumamosi December 10 2016 na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 40.
Taarifa iliyotolewa mapema leo December 11 2016 asubuhi na msemaji wa idara ya taifa ya mambo ya dharura nchini Kenya Pius Masai amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo na kwamba magari zaidi ya 11 yameteketezwa kwa moto katika barabara ya Nairobi-Naivasha.
Maafisa kutoka wizara ya usafirishaji wakiongozwa na Katibu mkuu wa wizara hiyo Irungu Nyakera
wamewasili katika eneo la tukio na Taarifa zaidi zinaeleza kuwa watu
wengi wamejeruhiwa na miongoni mwao ni watu waliokuwa wakirejea nyumbani
kutoka harusini subukia.
Katibu mkuu Irungu amesema kuwa kwa
uchunguzi wa awali umebaini kuwa ajali hiyo imetokana na dereva
kutokufahamu vizuri barabara hiyo kutokana na kwamba lori hilo la mafuta
ni la nchini Uganda.
millardayo
No comments:
Post a Comment