Korogwe, WANANCHI kijiji cha Makinyumbi
Miembeni kata ya Hale Wilayani Korogwe Mkoani Tanga wameutaka uongozi wa kijiji
kuwasomea mapato na matumizi.
Wananchi hao
wamedai zaidi ya miaka miwili hawajasomewa mapato na matumizi Ilhali wako na vyanzo vingi vya mapato ikiwemo minara ya simu
na mazao mashambani.
Wakizungumza
kwenye mkutano wa wananchi kuzungumzia maendeleo ya kijiji, wananchi hao wamedai
kuwa kwa kipindi kirefu hawajasomewa mapato na matumizi jambo linarudisha nyuma
maendeleo ya kijiji.
Wamesema kufikia
hatua hiyo watapeleka malalamiko yao kwa Waziri
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kutaka
kutumwa wataalamu wa fedha kwa uchunguzi.
“Ni miaka
miwili hatujasomewa mapato na matumizi nah ii inatia shaka kwani tunajua kuwa
ukusanyaji ushuru wa mazao na kodi za wawekezaji zinaendelea kukusanywa”
alisema Benantula Alphonce na kuongeza
“Kijiji
chetu kiko nyuma kimaendeleo na huduma za kijamii na tumeshindwa hata kuweka
zahanati angalau kuwaepushia kero wajawazito na wazee kufuata matibabu masafa
marefu” alisema
Mwenyekiti
wa kijiji hicho cha Mwakinyumbi Miembeni, Erica Bahati, alisema hana hoja
yoyote ya kujibu kero hizo kwa madai kuwa yeye sio msemaji wa kijiji.
Alisema
hawezi kuzungumza na waandishi wa habari kwa vile hana taarifa za ujio wao na
kibali cha kuingia kijijini hapo hivyo kuwataka kuwafuta waliowaita.
‘Mimi siwezi
kuzungumza chochote kwani sio msemaji wa kijiji na pia ninyi mumefikaje hapa
wakati hamna kibali na nani amewaita hadi kufika kwangu” alisema Bahati
Aliwataka
waandishi hao pamoja na mwandishi wa habari hizi kufuata taratibu za kuchukua
habari katika maeneo na kuweza kupata habari kwa kina ambazo zitasaidia
kusukuma maendeleo ya wananchi.
Mwisho
Mkazi wa Korogwe Mkoani Tanga, Abdalla Jumanne, akitoa kero yake wakati mkutano wa wananchi uliofanyika jana kuzungumzia maendeleo na changamoto wanazokabiliana nazo.
Mkazi wa kijiji cha Makinyumbi Miembeni kata ya Hale Wilayani Korogwe Mkoani Tanga, Solomoni Hassan ju , akizungumza mbele ya wananchi wa kijiji hicho kuzungumzia kero mbalimbali wanazokabiliana nazo ikiwa na pmoja na kijiji kutosomewa mapato na matumizi.
Mkazi wa kijiji cha Makinyumba Miembeni kata ya Hale Wilayani Korogwe Mkoani Tanga, Ester John, akitioa kero yake mbele ya wananchi wa kijiji hicho ikiwemo uhaba wa maji na kufuata matibabu masafa marefu.
No comments:
Post a Comment