Thursday, December 15, 2016

MADHARA YA MATUMIZI YA MIRUNGI ( MIRAAA)

MADHARA YA MATUMIZI YA MIRUNGI KIAFYA

Mtumiaji wa mirungi yupo katika hatari ya kupata vidonda vya tumbo.

  1. Kupungukiwa msukumo wa kufanya tendo la ndoa (low sex drive) na pia kuwahi kumaliza haraka na kutoweza kudumu kwenye tendo la ndoa kwa muda mrefu.
  2. Ukosefu wa haja kubwa (constipation)
  3. Utumiaji wa muda mrefu husababisha ini kushindwa kufanya kazi, pia meno kubadilika rangi, kudhoofika, fizi kuuma na harufu mbaya mdomoni.
  4. Upungufu wa usingizi.
  5. Humpelekea mlaji kutawaliwa nayo. (addiction)
  6. Madhara ambayo bado kinamama walaji Mirungi hawajagundua ni kwamba mtoto anayezaliwa na mama mlaji Mirungi mara nyingi hukataa kunyonya titi la mama yake kwa sababu ladha ya maziwa inabadilika kwa ajili ya utumiaji wa madawa (pesticides) unaotumiwa na wakulima wa Mirungi kama inavyoeleza utafiti uliofanyika na Chuo Kikuu Cha Aden (Aden University).
  7. Utafiti mwengine kule Ethiopia unatueleza ya kuwa mtoto wa mama mwenye kula Mirungi kwa wingi huwa hana uzito wa kawaida wakati wa kuzaliwa.
  8. Ukosefu wa hamu ya kula chakula.
  9. Magonjwa ya vidonda vya tumbo (ulcers).
  10. Kupatwa na ugonjwa wa futuru/futuri/bawasiri/baasili - nyama inayoota kwenye utupu wa nyuma.
  11. Walaji wengi huvuta na sigara, hata yule aliyekuwa havuti kabla ya kuanza kula Mirungi, hujikuta akizama kwenye uvutaji, na madhara huwa maradufu.

No comments:

Post a Comment