Thursday, December 29, 2016

MAFURIKO YAUA WATU 50 KONGO

Mafuriko yawauwa watu 50  DRC  KONGO

Mafuriko nchini DR CongoTakriban watu 50 wamekufa na wengine maelfu kadhaa wameachwa bila makazi baada ya mafuriko makubwa kutokea kusini magharibi mwa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.
Mvua kubwa iliyonyesha maeneo hayo imesababisha kufurika kwa mto Kalamu, ambao ulimwaga maji katika mji wa Boma, ulipopasuka kingo zake Jumanne.
Miili ya waliokufa ilisombwa kwa maji hadi nchi jirani ya Angola, amesema gavana wa eneo hilo.
Wakazi wanasema baadhi ya maeneo ya mji huo yamezikwa ndani ya matope.
" Kwa kawaida maafa kama haya hutokea kila baada ya miaka 10.
Mara ya mwisho yalitokea mwezi Januari 2015, lakini kutokana na mabadiliko ya tabia nchi yametokea sasa mwezi Disemba 2016," Jacques Mbadu, gavana wa jimbo la Kongo ya kati (Congo Central province), ameliambia shirika la habri la AFP.
Maji ya mto Kalamu yalijaa kimo cha mita mbili (futi sita) juu ya kimo chake cha kawaida , aliongeza.
Mafuriko makubwa, ukame na gharika vinatarajiwa kuongezeaka kutokana na mabadiliko ya tabia  barani Afrika.

No comments:

Post a Comment