Wednesday, December 21, 2016

MTI AINA YA MKUNGU WAANGUKA NA KUBONDA GARI ILIYOKUWA IMEEGESHWA


Askari wa kikosi cha Jeshi la  Zimamoto na Uokozi Tanga akikata mti aina ya mkungu uliouangukia gari aina ya Toyota Allion mtaa Maktaba na kuvunja kioo na buti la nyuma tukio lililotokea jana saa 6.
Mti huo ulioko karibu na Jengo ka Ofisi za Uhamiani na Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga ulianguka na kusababisha taharuki kwa watumiaji wa njia hiyo.
Mbali ya kuanguka mti huo wakati  wakazi wa eneo hilo wakiangalia madhara mabaki ya mti huo ulianguka tena na kusababisha taharuki na watu kukimbizana na wengine kukanyagana.




Kwa habari, elimu na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment