Tangakumekuchablog
Tanga, MICHEZO ya tano ya Mamlaka ya
Usimamizi wa Bandari Tanzania (INTERPORTS GAMES) yamemalizika kwa timu ya
Bandari ya Tanga kuibuka Mabingwa wa jumla.
Timu ya
Bandari ya Tanga imeibuka kwa kunyakua vikombe 7 ikifuatiwa na Bandari Makao
Makuu Dar es Salaam kwa kujinyakualia vikombe 7 ambapo Bandari Mtwara na
Bandari za Maziwa kila mmoja kujinyakulia kikombe kimoja kimoja.
Akikabidhi
vikombe na zawadi mbalimbali kwa washindi Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya
Usimamizi wa Bandari Tanzania, Mussa Msabimana ,aliwapongeza washiriki hao kwa
kuonyesha umahiri katika michezo mbalimbali.
Alisema
mbali ya umri wao kwenda juu lakini walikuwa wakionekana kama vijana ambao
wanaweza kucheza timu yoyote inayoshiriki ligi kuu Tanzania Bara.
“Nimefarijika
kuwaoma wafanyakazi wenzangu umri tofauti mukicheza mpira na kushindwa
kutofautisha kijana na mzee, munakimbia uwanjani kama Messi na Ronaldo” alisema
Msabimana
Aliwataka
wanamichezo hao ambao ni watumishi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania
kuwa wamoja na kuwa na mshikamano ili kuweza kuyafikia malengo waliojiwekea.
Msindi wa
bao kutoka Bandari Makao Makuu Dar es Salaam, Mwinyi Sultan, akikabidhiwa kombe
na Kaimu Mkurugenzi wa Mmlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania, Mussa Msabimana
baada ya kuibuka msindi wa mchezo huo wakati wa michezo iliyofanyika Tanga kwa
siku 4 viwanja mbalimbali Mkoani humo.
Wachezaji wa timu ya Bandari Tanga michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, Netboll, kurusha Tufe, kuvuta kamba na riadha wakishangilia ushindi wa jumla mara baada ya kukabidhiwa kombe lao na Kaimu Mkurugenzi Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Mussa Msabimana. Bandari Tanga imeibuka mshindi wa jumla na kunyakua vikombe 6.
Wachezaji wa timu ya Bandari Makao Makuu Dar es Salaam wakishangilia ushindi mara baada ya kukabidhiwa vikombe vyao kwa michezo mbalimbali, Bandari Makao Makuu walinyakua vikombe 7.
Raha ya Ushindi Bandari Mkao Makuu.Dar es Salaam,
No comments:
Post a Comment