Thursday, December 15, 2016

MAJI YA KALE YAGUNDULIWA CANADA

Maji ya kale zaidi duniani yagunduliwa Canada

WMgodiWanasayansi nchini Canada wamegundua maji yanayoaminika kuwa ya kale zaidi duniani, ambayo wanaamini yamekuwepo angalau kwa miaka bilioni mbili.
Maji hayo yamegunduliwa katika mgodi uliopo nchini Canada.
Wanasayansi walikuwa wamegundua maji mengine mwaka 2013 eneo hilo yaliyokadiriwa kuwa ya kutoka miaka 1.5 bilioni iliyopita lakini sasa wanasema maji waliyoyagundua karibuni ni ya zaidi ya miaka milioni mbili iliyopita.
Wanasayansi hao kutoka chuo kikuu cha Toronto waliwasilisha matokeo ya utafiti wao katika mkuano wa wataalamu wa fizikia ya dunia mjini San Francisco.

No comments:

Post a Comment