Saturday, December 24, 2016

NDEGE ILIYOTEKWA LIBYA YATUA MALTA

Ndege iliyotekwa nyara nchini Libya yatua Malta

Ndege hiyo ilikuwa safarini ndani mwa Libya
Ndege  ya Libya iliyoripotiwa kutekwa nyara ikiwa kwenye safari ya ndani ya nchi imetua nchini Malta.
Ndege hiyo aina ya Airbus A320 ya shirika la ndege la serikali ya Libya, Afriqiyah, ilikuwa na abiria 118 wakati ikitekwa.
Watekaji nyara wawili waliripotiwa kutishia kuilipua ndege hiyo.
Ndege hiyo ilikuwa safarini kutoka mji wa Sebha kusini magharibi mwa Libya ikielekea mji mkuu Tripoli kabla ya kuelekezwa nchini Malta, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters.

No comments:

Post a Comment