Ligi ya soka DR Congo yasitishwa
Ligi ya kandanda
nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DR Congo) imesitishwa kwa muda
usiojulikana kutokana na sababu za kiusalama.
Serikali ililitaka shirikisho la soka nchini humo kusitisha mechi za ligi kuanzia Alhamisi.Hatua hiyo imetokea huku wasiwasi ukiendelea kwamba huenda kukatokea vurugu muhula wa Rais Joseph Kabila utakapofikia kikomo wiki ijayo.
Majuzi wakati wa mechi, mashabiki walisikika wakiimba kwamba muhula wa Kabila unamalizika.
Kabila alitakiwa kung'atuka 19 Desemba lakini amesema anapanga kusalia madarakani hadi Aprili 2018, wakati ambao serikali inasema itaweza kufanya uchaguzi ambao ulikuwa umepangiwa kufanyika mwezi jana.
BBC
No comments:
Post a Comment